Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo katika kiwanja cha Shule ya Msingi Wichamike kata ya Ntobo Halmashauri ya Msalala ukitokea Halmashauri ya Ushetu ndani ya wilaya ya Kahama.
Mwenge huo umepokelewa na kulakiwa na maelfu ya wananchi katika kiwanja hicho huku vikundi mbalimbali vikiendelea kutumbuiza na kufanya hamasa,awali Mkurugenzi Mtendaji(W)
Ndg.Khamis Jaaphar Katimba akipokea mwenge huo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji(W) Halmashauri ya Ushetu, amesema "Mwenge wa Uhuru utakimbizwa KM.70 na utazindua na kuwekea
mawe ya Msingi miradi 5 ndani ya Halmashauri, miradi hiyo ni ya maji na mazingira katika kijiji cha masabi, Afya na elimu katika kijiji cha Segese na kuona shughuli za vijana
wanaotegeneza masofa Kakola ambao wamenufaika na 10% ya mikopo ya mapato ya ndani na baadae mwenge utaelekea viwanja vya kakola A na B kwa ajili ya risala ya Utii na Mkesha na
siku itakayofuata utakabidhiwa Halmashauri ya Nyagwale Mkoani Geita".
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amesema," mwaka 2022+23 Serikali ilitoa Tsh.2,047,466,386 kwa sekta ya Elimu ambapo madarasa 54,nyumba 5 za walimu,bweni 1 la wana
funzi wenye mahitaji maalum na matundu ya vyoo 220 na madawati 810 yametengenezwa kwa fedha hizo, Tsh. 750,000,000 zimetolewa katika idara ya afya kwa ajili ya ujenzi wa jengo
la mionzi,upasuaji, wodi ya wanaume na jengo la kufulia na kupanda miti 1500 kuzunguka hospitali ya wilaya ya Halmashauri hiyo.Halmashauri imekusanya Tsh. 5,167,635,017 sawa na
103% ya kukusanya Tsh.4,532,000,000 kwa mwaka huo.Katika sekta ya Ujenzi Halmashauri imetumia Tsh. 2,667,290,000 TARURA kufanya matengenezo ya barabara ndani ya Halmashauri.
Fursa zilizopo ni Umeme, Maji, Usafiri muda wote,nguvu kazi kwa wananchi, mashirika mbalimbali,ardhi yenye rutuba, machimbo ya dhahabu kwa wachimbaji wadogo wadogo na amehitimi
sha kwa kutoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na DR.Samia H. Suluhu kwa kuunga mkono jitihada za wananchi kwa kutoa mabilioni ya fedha kukamilisha miradi katika
sekta mbalimbali.
upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Ndg.Abdalla Shaib Kaim amefurahishwa na mwamko wa wananchi wa jimbo la Msalala kwa kuwa kila sehemu walipopita (miradi waliyotembelea)
walikuta umati mkubwa wa wananchi wakiusubiria Mwenge wa Uhuru, kiongozi huo amesifu wananchi wa Halmashauri hii na kuwaomba kuendelea na moyo huo wa kizalendo. Sambamba na hilo
kiongozi huyo na jopo lake wameridhishwa na miradi yote waliyoipitia na kusema"miradi ni mizuri sana na ni ya kiwango cha juu" pongezi kwa Rais Dr.Samia Suluhu kwa kuthamini wananchi
kwa kutoa fedha kwa ajili ya sekta mbalimbali nchini zenye lengo la kuhakikisha maendeleo na ustawi wa jamii unakuwepo kwani mazingira ya kufikia maendeleo hayo tayari Serikali ya
awamu ya sita imeyatengeneza.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.