Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Christina Solomoni Mndeme wakati wa ziara ya kupitia miradi itakayozinduliwa na
Kuwekewa mawe ya msingi kwenye mbio za Mwenge ambao utapokelewa katika viwanja vya Shule ya Msingi Wichamike katika kijiji cha Ntobo
"A" kata ya Ntobo. Miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo Jumla ya Tshs. 632,820,000 itatumika hadi kukamilika kwa awamu ya kwanza.
Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa uhuru ni upanuzi wa maji ambapo vituo vinne vimejengwa katika kijii cha masabi, Shamba la miti na
Upandaji miti katika zahanati ya Masabi ambapo miti 500 itapandwa na mwenge huo, Ujenzi na uwekaji wa jiwe la Msingi katika Kituo cha
Afya segese ambapo hadi sasa jengo la OPD na Maabara vimekamika, Ujenzi wa bwalo la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi
Segese na mradi wa kikundi cha watengeneza sofa ambacho kilipatiwa Mtaji wa Tshs. 30,000,000 kama mkopo wa Halmashauri.
Mhe. Mndeme amesema yeye na timu yake ya Usalama Mkoa na Wilaya wameridhishwa na Miradi inayotekelezwa ndani ya Halmashauri
kwani Miradi hiyo imejengwa kwa viwango vya juu na kwa ufanisi, hii itawezesha miradi hiyo kudumu kwa muda mrefu. Pongezi kwenu Wananchi
wa Msalala hakika inaitendea haki ilani ya chama cha Mapinduzi inayotaka kuweka mazingira mazuri kwa uwekezaji na kuhakikisha jamii ina afya njema.
Mkuu wa Mkoa huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na MHE.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa
MHE.DR. Samia Suluhu kwa kuunga mkono miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri kwani miradi ya maji, ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wenye
mahitaji maalum,Elimu na afya MHE.Rais ametoa fedha nyingi kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.