HALMASHAURI YA MSALALA YAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI KWENYE KILIMO
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ndg Zainabu Terack iliyofanyika ndani ya Halmashauri ya Msalala iliyo kuwa na lengo la kutembelea na kukagua namna shughuli za kilimo zinavyoendelea ndani ya Halmashauri hiyo na kujioneo jinsi wakulima walivyo hamasika kwa kiasi kikubwa kulima mazao ya chakula na biashara kwa wingi . Pia Mkuu wa Mkoa alijionea Mashamba Mbalimbali ya Alizeti, Karanga, Mahindi na Pamba.
Mkuu wa Mkoa alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Simon Berege pamoja na timu nzima ya Maafisa Ugani wa Halmashauri ya Msalala kwa kazi nzuri waliyo fanya ya uhamasishaji wa kilimo cha kisasa kwa wakulima na kuwahimiza kutoa elimu ya kutosha kwa Wakulima ambao bado hawajahamasika ili nao waige mfano mzuri toka kwa wenzao waliolima kilimo cha kisasa.
Sambamba na hilo pia Mkuu wa mkoa alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya Wakulima ambapo walitoa changamoto zao kwa Mkuu wa Mkoa huyo, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na kipato cha kutosha kununua pembejeo za kilimo na hivyo kushindwa kuhudumia mashamba yao vizuri. Mkuu wa Mkoa aliwashauri wakulima hao kuwa watumie mbolea za kupandia na kukuzia ili waweze kuvuna mazao ya kutosha kwani Serikali ilishatoa ruzuku kwenye mbolea na hivyo mbolea zimeshuka bei ukilinganisha na kipindi cha nyuma , pia watumie dawa za kuulia wadudu waharibifu (viuwadudu) aina ya DUDU BA 450 ec iliyo na uwezo mzuri wa kupambana na wadudu wahalibifu. Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa Afisa ugani wa Halmashauri ya Msalala Ndg.Solomon Zedekia alisema kuwa Wananchi wa Halmashauri ya Msalala wamelima kiasi cha heka elfu therathini kwa mwaka huu wa kilimo na hivyo kufikia malengo ya Halmashauri.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.