HALMASHAURI YA MSALALA YAPONGEZWA KWA KUWA NA HUDUMA NZURI ZA AFYA
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Zainab Telaki ilifanyika katika kata tatu (3) za Halmashauri ya Wilay ya Msalala , ambapo vituo vya Afya viwili vilitembelewa na zahanati moja. Lengo la ziara hiyo lilkuwa ni kuangalia namna huduma za Afya zinavyo tolewa sambamba na uhamasishaji jamii kujiunga na mfuko wa bima ya jamii(CHF iliyo boreshwa)
Akikagua vituo vya Afya vya Chela na Bugarama Mkuu wa Mkoa Mh. Zainabu Telack alilidhishwa na namna huduma za Afya zinzvyo tolewa katika vituo hivyo sambamba na upatikanaji wa madawa kwani vituo vya afya ndani ya Halmashauri ya Msalala vilikuwa na akiba ya kutosha ya dawa muhimu
Akipokea taarifa ya kituo cha afya cha Chela Mh.Telack aliutaka uongozi wa kituo hicho kuelimisha jamii ili kuchangia damu salama kwa lengo la kuokoa maisha ya akina mama wajawazito.
Mkuu wa mkoa pia alikabidhi vitambulisho vya Wazee 137 katika kata ya Bugarama na akihitimisha ziara yake katika kijiji cha Segese ambapo alihimiza jamii ya wakazi wa Segese kujiunga na mfuko wa CHF iliyo boreshwa kwani ni mkombozi wa maisha kwakuwa magonjwa hutokea pasipo taarifa. Mkuu wa mkoa aliwalipia kaya 20 zenye wanacha 120 zoezi lililo ungwa mkono na Mh. Diwani wa kata hiyo Mh. Joseph manyara ambaye alilipia kaya 2 zenye wanachama 12 na hivyo wanachama waliojiandikisha katika mfuko wa CHF kuwa kaya 22 zenye wanachama 132
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.