HALMASHAURI YA MSALALA YAPONGEZWA KWA UTOAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amefanya ziara ya siku moja katika halmashauri ya Msalala ambayo ni moja kati ya Halmashauri iliyofanya vizuri katika utekelezaji wa mpango wa malipo kwa ufanisi (RBF) kwa kutembelea katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma na kujionea utekelezaji huo ukifanyika ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi wa Msalala.Pia amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Msalala Ndg. Simon Berege kwa usimamizi mzuri kwa watendaji wake wa idara ya Afya na wakiongozwa na mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk. Tom Mtoi na kupelekea kuwa na ufanisi katika utoji wa huduma za afya na kufanya kuwa bora. Akizungumza mbele ya wananchi na waandishi wa habari Waziri Umi Mwalimu alisema kuwa bajeti ya ununuzi wa dawa umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye uongozi wa awamu ya tano ukilinganisha na uongozi wa awamu ya nne ambapo awamu ya nne bajeti kwaajili ya ununuzi wa dawa ilikuwa ni kiasi cha Tsh. Milioni miamoja na nane(108,000,000) ukilinganisha na bajeti ya ununuzi wa dawa kwa sasa ni zaidi ya Tsh. Milioni mianne (400,000,000). Pia alijionea uwepo wa dawa za kutosha ambao unapelekea kupungu kwa kelo za upungufu wa dawa uliokuwa ukiwapata wagonjwa. Pamoja na hayo Waziri Umi alimpongeza Mkurugenzi Kwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha za RBF na kusema kuwa fedha hizo zimetumika vizuri na kwa wakati na hivyo kusisitizwa kuendelea kuwa wabunifu ili wananchi waendelee kupata huduma bora za afyatamisemi
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.