Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama imeweka malengo ya kukusanya Tsh. Bilioni 7 katika mwaka mpya wa fedha 2024/25 ambapo kwa mwaka uliopita ilikusanya Tsh. Bilioni 6 na milioni 300 na kuvuka
lengo la kukusanya Bilioni 5.7 ambapo imekusanya zaidi ya milioni 600 hadi kufikia leo tarehe 27.06.2024.Takwimu hizi zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji(W) bwana Khamis Katimba wakati wa kikao cha
kufanya Tathmini ya mwaka wa fedha 2023/24 na kuweka malengo kwa mwaka ujao 2024/25.
Kikao hicho kimejumuisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama,Maafisa Tarafa wa Tarafa za Msalala na Isagehe,Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri,Watendaji wa kata na vijiji wote wa Halmashauri hiyo.
Lengo la kikao ni kutathmini yaliyofanyika mwaka 2023/24 na kuweka malengo kwa mwaka 2024/25 sambamba na kukumbushana wajibu wa watumishi wa umma kwa jamii wanazoziongoza.Katika kikao hicho mada mbalimbali
zimewasilishwa zikiwemo ukusanyaji mapato,utawala bora,mipango na bajeti na maandalizi ya uchaguzi wa wenyeviti.
Bwana Katimba amesema mapato ndio uti wa mgongo wa Halmashauri na sisi ndio injini ya kuhakikisha mapato halali ya Halmashauri yanakusanywa,hakikisheni mianya yote ya upotevu wa mapato ya Halmashauri
inazibwa na fedha inakusanywa,sina shaka na ongezeko la bajeti tulilopatiwa kwani kupitia vikao ninavyovifanya mara kwa mara nanyi,wenyeviti wa vijiji na vitongoji na Waheshimiwa madiwani.Nina uhakika
Bilioni 6.7 zinakusanyika nami naongeza milioni 300 ili tukusanye Bilioni 7.
Nae Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu NDG.Mang'era amewataka watumishi kuwa wabunifu kwa kuweka na kusimamia kikamilifu mpango na bajeti ili miradi itakayopitishwa ngazi za kata ziwe na tija katika utekelezaji
wake kwani wao ndo wataalamu katika maeneo yao hivyo watumie elimu zao kuleta mabadiliko chaya ndani ya kata na Halmashauri kwa ujumla.Tumefanya vizuri mwaka huu tunaoumaliza siku si nyingi naomba
changamoto zilizojitokeza iwe fundisho kwa mwaka ujao ili tufanye vizuri zaidi na simamieni miradi yote inayotekelezwa penye changamoto tuwasiliane mapema.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Utumishi na Raslimali watu NDG.Mary Nziku amewataka watumishi ndani ya Halmashauri kufanya kazi kwa bidii na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita Inayoongozwa na
DR.Samia Suluhu na kutaka kero zote zitatuliwe kwa wakati kwani sisi tu karibu na jamii,hakikisheni vikao vyote vya kisheria vinafanyika na mihtasari ya vikao hivyo zinaletwa Halmashauri,Mkurugenzi ameweka mlezi
kwa kila Kata lengo ni kuhakikisha yanayojadiliwa katika maeneo yenu yanafika Halmashauri kwa wakati na Halmashauri kuyafanyia kazi kwa wakati.
Akihitimisha kikao hicho,Katibu Tawala Bi.Jackline amewataka watumishi kufuata sheria,kanuni na taratibu katika utendaji kazi wa kila siku ili kuepusha migogoro isiyokuwa na ulazima,fuateni miongozo katika
ukusanyaji mapato sambamba na kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwa watendaji wa vijiji pindi watakaposimamia ofisi za vijiji pasipo kuwa na wenyeviti wa vijiji.Mwaka huu tuna uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji
na vitongoji hamasisheni wananchi kujitokeza kuboresha taarifa zao na baadae kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wanaowahitaji kwa kuwa ni haki yao kuchagua viongozi.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.