Halmashauri ya Msalala imefanya maajabu makuu kwa kutoa fedha za mikopo kwa zaidi ya 10% kwa mwaka wa fedha 2021 kwa wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wazee. Katika mwaka 2020/2021 Halmashauri hiyo ilitoa milioni 256 ambazo milioni 206 ni michango iliyotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani na milioni 50 ni marejesho ya vikundi vilivyokopeshwa. Kauli hiyo imetamkwa na Mkurugenzi Mtendaji (W) bwana Edward C. Fussi katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, ambapo amesema Halmashauri imeshika nafasi ya pili kitaifa kwa utoaji wa mikopo kwa vikundi vilivyokidhi vigenzo vilivyowekwa.
Wakichangia hoja katika mada hii Waheshimiwamadiwani wameipongeza Halmashauri kwa kufanya vizuri katika eneo hili na kuomba wataalamu wa idara ya maendeleo ya Jamii kuielimisha zaidi jamii kwani pamekuwepo na malalamiko ya baadhi ya vikundi kutopatiwa taarifa licha ya kuomba mikopo hiyo, suala ambalo Mkuu wa idara hiyo Bi Neema katengeshya ameahidi kuufanyia kazi ushauri huo. Pia mkuu wa idara hiyo ameongeza pia wananchi wengi wamehamasika na hivyo vikundi vingi vinaomba lakini fedha inayotengwa licha ya kuwa zaidi ya 10% lakini bado haitoshi hivyo kuomba wadau kujitokeza ili kuunga mkono jitihada za serikali.
Waheshimiwa Madiwani wamezungumzia suala la kupewa taarifa za mradi wowote utakaofanyika ndani ya eneo la kila diwani kwani kumekuwepo na tatizo la waheshimiwa kutopewa taarifa hasa kwa miradi inayotekelezwa na wadau wa maendeleo, suala ambalo Mkurugenzi Mtendaji (W) ameahidi kuhakikisha taarifa zinatolewa kwa Mh. Diwani, Mtendaji wa kata na kijiji, mwenyekiti na wananchi.
imetolewa na kitengo cha TEHAMA Halmashauri ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.