Imeelezwa na kusisitizwa mtoto ni lazima anyonyeshwe muda wa miaka 2 na kupatiwa vyakula vyenye mchanganyiko wa makundi yote yq vyakula
vikiwemo wanga,protini,matunda,mbogamboga,sukari kiasi na mafuta mara 5 kwa siku ili kuwezesha ukuaji wake na kumuondolea uwezekano wa kushambuliwa
na magonjwa,kauli hiyo imetolewa na Afisa Lishe mkoa wa Shinyanga Bwana Yusuph Hamis wakati wa kikao cha kujadili mpango na bajeti wa Kamati yaLishe ya
Halmashauri ya Msalala.
Awali akifungua Kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba amewaomba wajumbe kufuatilia kwa makini mafunzo hayo kwani baada ya muda si mrefu
yatatumika katika mipango na bajeti ya Halmashauri,pia lishe ni suala mtambuka ambalo kila mtu anapaswa kufahamu kwa undani na kufanyia kazi kwenye
familia au jamii inayomzunguka.Tutaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwezesha elimu kutolewa kwa jamii kwani ndani ya Halmashauri yetu naona mila na
desturi zina nguvu na kusababisha watoto chini ya miaka 5 kutopewa haki zao za msingi na hivyo kupelekea udumavu.
Akiwasilisha Mpango na Bajeti wa lishe kwa mwaka 2024-25,Afisa Lishe wa Halmashauri ya Msalala Bi,Mwamini Mziray amesema jamii imehamasika juu ya unyonyeshaji wa watoto
chini ya miaka 5 na kuomba kutilia mkazo suala la kula mbogamboga na matunda hasa kwa kinamama na watoto kwani kumekuwepo na changamoto ya upungufu wa
damu na matumizi ya chumvi isiyokuwa na madini joto hivyo ameiasa jamii kuhifadhi chumvi yenye madini joto sehemu salama mara baada ya kuifungua na kuitumia.
Sambamba na hili ametoa wito kwa shule kuendeleza kilimo cha mbogamboga na mahindi-mpunga ili kuwezesha wanafunzi kupata chakula cha asubuhi na mchana.
Bi,Mwamini Mziray amesema Mpango na Bajeti kwa mwaka 2024-25 umelenga kutatua changamoto zilizoonekana kwa mwaka 2023-24 na kuomba kwa pamoja kushirikiana
katika kuhakikisha elimu na mafunzo kwa vitendo yanatolewa katika maeneo yote ya utawala ndani ya Halmashauri kupitia warsha kwa jamii,vyombo vya habari na
kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwani wana mchango mkubwa katika kufanikisha shughuli hii kwa kuwa wapo karibu na jamii na huishi maeneo ya jamii.
Masuala ya kupunguza utapiamlo,uzito mkubwa,upungufu wa madini kama Vitamini A,matumizi ya vyakula vilivyoongezewa lishe,matibabu kwa waathirika wa utapiamlo
yatolewe hasa katika vituo vya afya viongezwe ili waweze kupatiwa matibabu na kujenga mazingira wezeshi kwa wataalam kuweza kutembelea maeneo yenye changamoto.
Washiriki wametoa rai kwa wawezeshaji kutekeleza mpango wao kama ulivyo na kuahidi kutoa ushirikiano na kuomba watumishi waliopo ngazi za kata na vijiji washirikishwe
suala ambalo limekubaliwa.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.