Jitihada za MHE. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR. Samia H. Suluhu
zimeungwa mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala MHE. Mibako Mabubu
ambae ametoa gunia 67 za mahindi na kuhamasisha wadau wa Chela nao kuchangia
gunia 7 za Mahindi hivyo kufanya jumla ya magunia ya mahindi 74 kutolewa.
Tafrija hii imeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama MHE. Mboni Mhita aliyeongozana
na Mkurugenzi Mtendaji(W) ndugu Khamis J. Katimba, MHE.Joseph S. Luyombya Diwani
wa Kata ya Bulyanhulu, Kaimu Afisa Elimu Awali na Msingi(W),
Wataalamu mbalimbali wa ngazi ya kata na wadau wa maendeleo kata ya Chela.
Mkuu wa Wilaya ameitaka jamii kufuata mfano ulioonyeshwa na kiongozi wetu.
Magunia hayo yametolewa katika shule za Msingi na Sekondari za kata ya Chela
ambapo Mgeni rasmi MHE. Mboni Mhita amekabidhi mahindi hayo kwa wanafunzi na
walimu wa shule hizo. Awali akisoma taarifa ya makabidhiano hayo Mtendaji wa
Kata ya Chela Bi.Evagsira amesema mgawanyo wa mahindi umezingatia wingi wa
wanafunzi katika shule husika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri, amesema yeye akiwa kama mzazi
ameshawishika kuunga jitihada za Rais wetu DR. Mama samia suluhu Hassain
kwani MHE. Rais amefanya mengi mazuri ikiwemo kujenga majengo ya kisasa
mashule na hospitalini sambamba na kutoa ajira katika sekta za Afya na
Elimu, pia kitu kingine kilichomvutia ni mwitikio wa wanachela kwani wengi
walijitokeza kuchangia huduma ya watoto kupata chakula shuleni muda wa masomo.
Nae Mbunge wa Jimbo la Msalala MHE. Iddi Kassimu Iddi ameunga mkono Jitihada za
mwenyekiti huyo kwa kutoa mifuko ya sukari 12 ambazo zimekabidhiwa katika tafrija
hii.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.