Jitihada za kuwaletea maendeleo Watanzania zinazofanywa na MHE. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kujenga hospitali na kuhakikisha zina vifaa muhimu kwaajili ya afya za wananchi, shule kwa ajili ya
kuelimisha watoto na kuwalinda na athari mbalimbali za kimaadili ndani ya jamii zimeungwa mkono na taasisi
mbalimbali za kimataifa zikiwemo UN-WOMEN, UNFPA na KOICA.
Mashirika haya yamewezesha Ujenzi wa kituo kimoja cha huduma shufa (one stop center) katika kituo cha Afya
Bugarama inayopatikana katika kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama pia yamewezesha ujenzi
wa ofisi ya dawati la Jinsia na watoto( Police Gender and Children Desk) katika kituo cha polisi Bugarama.
Majengo haya yamezinduliwa na MHE. Mkuu wa Wilaya ya Kahama MHE. Mboni muhita ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga katika hafra hii. Hafra hii imehudhuliwa na viongozi mbalimbali kutoka UN-WOMEN, UNFPA, KOICA, Jeshi
la Polisi nchini hasa wanaoshughulikia masuala ya dawati la Jinsia na watoto, OR-TAMISEMI, Kamati za ulinzi na
Usalama Mkoa wa Shinyanga na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Kahama, WAH. Madiwani wakiongozwa na MHE. Manyara
Wataalamu toka ngazi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Msalala.
Akiwakaribisha wageni mbalimbali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala ndg. Charles Fussi amesema mashirika haya
yamefanya mengi ndani ya Msalala ikiwemo mafunzo kwa maafisa polisi 20, maafisa kilimo 125 wa Halmashauri,
vikundi 60 vya wakulima vimepatiwa mafunzo ya ujasiriamali, kuongeza uelewa kwa jamii kupambana na unyanyasaji
na kuwezesha vikundi 10 kufunga umeme jua ili kuwa na uhakika wa kulima mwaka mzima. Sambamba na haya mkoa wa
wa Shinyanga umepatiwa gari 2 kupitia mradi huu ambapo gari moja ipo Halmashauri ya Msalala na nyingine Mkoani.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.