Shughuli za kiuchumi wilaya ya Kahama hususani ndani ya Halmashauri ya Msalala 31.10.2023 zilisimama kwa muda kufuatia ufunguzi wa jengo la Utawala la Halmashauri
hiyo lililopo katika kijiji cha Buganzo pembezoni mwa barabara kuu itokayo Kahama kwenda Kakola,Jengo hilo limejengwa kwa thamani ya zaidi Tsh.bilioni 3 fedha kutoka
Serikali kuu,pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha kukamilika kwa wing ya kwanza ya jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.Sherehe hiyo umehudhuriwa
na kamati ya ulinzi na usalama(W) ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe.Mboni mhita ambaye pia ni mgeni rasmi kwenye hafra hiyo,Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe.
Alhaj Idd Kassim Idd,viongozi wa chama na Serikali,Waheshimiwa Madiwani,wataalamu wa halmashauri na taasisi mbalimbali na wananchi wa kata za Ntobo,Mega na Segese.
Akifungua hafra hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe.Mibako Mabubu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Samia Suluhu kwa kuleta mabilioni ya fedha ndani
ya Halmashauri kutekeleza miradi mbalimbali hakika ameitendea haki Halmashauri haijawi kutokea miradi mingi kutekelezwa ndani ya muda mfupi tangu Serikali yake iingie
madarakani,tunashukuru sana sisi wananchi wa Msalala na tunaomba aendelee kutuunga mkono katika shughuli zetu za kila siku nasi tunaahidi kuwa nae bega kwa bega.
Akitoa hotuba kwa wananchi wa Halmashauri ya Msalala Mhe.Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama (W) Mhe.Mboni mhita amempongeza Mkurugenzi Mtendaji(W) wa Halmashauri
ya Msalala NDG.Khamis Katimba kwa kuwa na maono ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Halmashauri hiyo kwani anaunga mkono kwa vitendo jitihada zinazofanywa na Rais wetu
Dr.Samia Suluhu kwa kuhakikisha fedha zinazoletwa na Serikali zinafanya kazi kusudiwa na kukamilika kwa wakati na kuwaomba watumishi na wananchi kumpa ushirikiano.
Mkuu wa Wilaya huyo amempongeza pia Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe.Alhaji Idd Kassim Idd kwa kuthamini wananchi wake na kuwasemea mazuri kwa Mhe.Rais Dr.Samia Suluhu na
ndiyo maana mnaona miradi mingi ikitekelezwa,yote hii ni kazi ya Mhe.Mbunge wetu.Hongera sana Mhe. Idd Kassim Idd endelea kutuwakilisha vema bungeni na sisi wananchi wa
Halmashauri ya Msalala hatutokuangusha kwani tunaimani kubwa nawe kwa mazuri mengi uliyoyafanya ndani ya muda mfupi tangu uingie madarakani lakini kubwa zaidi ni kufanya
ziara za mara kwa mara vijijini na kutatua changamoto za wananchi.Utumishi wako si bure Mungu atakuinua.
Nae Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba amemshukuru Rais Dr.Samia Suluhu kwa kumwamini na kumpangia kazi katika kituo chenye viongozi mahiri,wanaojituma na wenye
mori ya kufanya kazi muda wote kwani tangu ameripoti ndani ya mkoa wa Shinyanga ushirikiano anaopata ni mkubwa na ndiyo maana unaona miradi ikitekelezwa kwa viwango na
ndani ya muda mfupi, yote hii ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya viongozi wa Chama,Serikali,Taasisi za umma,mashirika ya dini,Waheshimiwa Madiwani na wadau
mbalimbali ndani ya halmashauri.Mimi kiongozi mkuu wa Halmashauri ya Msalala nitawatumikia wananchi wa Msalala muda wote na nipo tayari kwenda sehemu yeyote kutatua kero
zao.
kwa Upande wake Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe.Alhaji Idd Kassim Idd amemshukuru sana mama wa taifa Dr.Samia Suluhu kwa upendo wake kwa wananchi wa jimbo la Msalala kwani
haijawahi kushuhudiwa miradi mikubwa na mingi kiasi hiki ikitekelezwa ndani ya Halmashauri ya Msalala kama inavyotekelezwa katika Serikali ya awamu ya sita,Mhe.Rais Samia
ametoa mabilioni ya fedha kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii kama ujenzi wa shule 2 mpya katika kata ya Bulyanhulu,VETA,mradi wa maji wa nduku busangi toka ziwa viktoria
,kuanza kwa matengenezo ya barabara ya lami kutoka Kakola kwenda Kahama katikati ya mwezi wa 11,hospitali ya wilaya na kukamilika kwa zahanati 23 haya yote ni baadhi ya mafanikio
ya Serikali ya awamu ya sita,tunaomba serikali utuletee wataalamu wa idara ya afya.
miundombinu imeshakamilika
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.