Kamati ya Lishe Halmashauri ya Msalala imejipanga kuhakikisha watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 na kina mama wajawazito ndani ya Halmashauri hiyo wanapata mlo uliokamilika muda wote, maneno hayo yamesemwa na Mratibu wa Lishe wa Halmashauri Bi. Mwamini Mziray katika kikao cha kufunga mwaka 2018/19 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mratibu huyo ameendelea kusema katika mwaka 2018/19 jumla ya wanawake 10,270 walipewa madini ya chuma na asidi ya Foliki, 13518 ya kinamama wenye watoto walio na umri chini ya miezi 6 wamepatiwa elimu ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi 6 na akinamama 17526 wenye watoto walio na umri kuanzia miezi 6 hadi miaka 2 wamepatiwa elimu ya ulishaji wa vyakula vya nyongeza kwa watoto.
Nao wajumbe wa kamati hiyo wamesema katika kipindi cha 2018/19 Halmashauri imefanya mengi yakiwemo kutoa elimu kwa jamii juu ya wanaume kuona umuhimu wa kuhudhuria kliniki na wenza wao pindi wanapokuwa wajawazito ambapo jamii imehamasika kwa kuongezeka kwa idadi ya kinababa kuhudhuria kliniki sambamba na kutoa hamasa kwa jamii kulima mazao ya chakula ili kuwezesha familia zao kujikimu kimaisha. Katika kufanikisha hili Taasisi isiyo ya Serikali ya AGPHAI imewezesha wanafunzi 240 kutoka kata za Lunguya, Ntobo, Segese na Isaka kupata chakula cha mchana. Halmashauri imewezesha jamii kujikinga na magonjwa kwa mifugo yao pamoja na kushauri jamii kuanzisha mabwawa kwa lengo la kufunga samaki ambapo tayari kuna mabwawa 3 ambayo yanafunga samaki.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) ndugu Zedekiah Solomon ametaka kila idara kuhakikisha mipango iliyojiwekea kuhusu Lishe yanatekelezwa kwani lishe ndio msingi wa kuwa na afya bora tuwe mfano kwa jamii ili jamii nayo ione umuhimu wa kuanzisha kilimo cha mazao yanayopatikana katika mazingira yao na amewapongeza idara ya Elimu kwa kuanzisha bustani za mbogamboga kwa lengo la kuwezesha wanafunzi kupata elimu ya namna ya kuanzisha bustani hizo majumbani mwao.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Halmashaur
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.