Kamati hiyo imetoa kauli hiyo kwenye kikao chake cha mwisho wa mwaka kilichofanyika leo tarehe 14/08/2018 makao makuu ya Halmashauri ya Msalala iliyoko katika kata ya Ntobo takribani kilomita 30 toka Kahama Mjini. Akifungua kikao hicho mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Alfed Mhanganya amewataka wah. Madiwani na wataalamu kushirikiana kwa ukaribu ili kuwaletea wananchi wa Halmashauri ya Msalala maendeleo kwani wao ndiyo viongozi na wataalamu katika masuala ya maendeleo ya wananchi.
Kaimu Afisa Kilimo amesema katika robo ya nne idara ya Kilimo, Ushirika na umwagiliaji imekusanya takribani kilo 400005 za pamba na kuhamasisha wananchi kuanzisha vyama vya ushirika kwa lengo la kupata bei nzuri za zao hilo suala ambalo kata 15 tayari zimeshaanzisha vyama hivyo, wajumbe wa kamati hii walipokea taarifa na kuomba wananchi wapewe elimu ya kutosha juu ya ufunguzi wa akaunti ya benki kama maelekezo ya Serikali yanavyotaka ili mzimu ujao wananchi waweze kulipwa fedha zao kupitia benki moja kwa moja.
Sambamba na hili wajumbe wameomba Serikali kuona naona bora ya kuwezesha kila kijiji kujenga ghala la kuhifadhia mazao kwani maeneo mengi wakulima wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hii, suala ambalo wakati mwingine linachangia kupoteza mapato kwa Halmashauri kwa kuwa wananchi walio mipakani na Halmashauri jirani hupeleka mazao yao kwenye Halmashauri zingine na hivyo mapato kuingia Halmashauri nyingine, ni vema Serikali ikawakopesha wanaushirika fedha ili wawezejenga maghala.
Kaimu mkurugenzi ndugu Zedekiah Solomon amesema ataongea na wadau hasa wanunuzi wa pamba ili kuona namna nzuri ya kufanya ujenzi wa maghala hayo kwani utaratibu uliopo sasa ununuzi wa pamba unafanywa na makampuni binafsi sambamba na kuomba wananchi wachangie nguvu kazi mara ujenzi wa maghala hayo utakapoanza. Pia ndugu Solomon ameongeza kusema idara ya Kilimo, ushirika na umwagiliaji imejipanga kuhakikisha kabla ya msimu wa mvua kutoa elimu juu ya kukabiliana na magonjwa ya mazao kama yaliyokuwepo katika msimu uliopita kwa kuwa idara hiyo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa.
Mwisho wajumbe wa kamati hii wameomba mwenyekiti na Mkurugenzi mtendaji wafikishe kilio chao cha usimamizi wa barabara kwa meneja TARURA kwani ukarabati unaofanywa maeneo mengi ya Halmashauri unafanywa katika hali duni kwa mfano mkandarasi anayefanya kazi barabara ya Lunguya Kalole (nyangalata) anatumia sululu kuchimba kifusi hivyo ni vema watu wa TARURA wafanye usimamizi wa mara kwa mara, sambamba na Serikali kuleta fedha ili maboma yaliyopo yaweze kukamilishwa kwa kuwa wanachi walihamasika kujenga maboma ni vema Serikali iwaunge mkono wananchi hawa.
Imetolewa na Kitengo cha Habari Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.