TAARIFA YA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA.
Wajumbe baraza la madiwani na wataalamu mbalimbali toka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ilipitia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Zoezi la ukaguzi wa miradi ya Maendeleo lilipitia jumla ya miradi 16 ya maendeleo ambayo ilighalimu jumla ya Fedha Tsh. 5,314 ,305,017 Ikiwa fedha kutoka mapato ya ndani ni Tsh. 187,500,000 na Tsh. 5,126,805,017 ni kutoka Serikali kuu na kwa wadau wengine wa maendeleo.
Wajumbe walilizika na ukamilifu wa miradi pamoja na mwendelezo wa ukamilishaji wa miradi ambayo nayo inaendelea kukamilishwa.
Wakaguzi walitoa maoni na mapendekezo ya kuanza kutumika kwa baadhi ya miradi ambayo imekwisha kamilika, ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii. Mfano wa baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na vyoo , barabara na machinjio ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Wajumbe walishauri wananchi washiriki kulinda na kuitunza miradi hiyo ili idumu kwa muda mrefu ili kuendelea kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma za kijamii. Pia walishauri kupanuliwa kwa barabara ya Busangi – Ntobo na kurekebishwa kwa madaraja ambayo yameonekana yameinuka sana .
Pia wakandarasi wanaojenga Makao makuu ya Halimashauri ya Wilaya ya Msalala walitakiwa kutoa ajira kwa vibarua wazawa wa maeneo husika ili kuongeza upatikanaji wa ajira .
Miradi ambayo haijakamilika, kamati walishauri wakandarasi wakamilishe miradi hiyo kwa wakati na pia Serikali ijitahidi kuwalipa wakandarasi kwa wakati.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.