Kampuni ya Colgate Palmolive East Africa LTD leo tarehe 16/05/2018 imekabidhi msaada wa dawa za mswaki katoni 97 na miswaki katoni 97 za
katoni 97 zote kwa pamoja zikiwa na gharama ya Tsh. 19555200. Akikabidhi Msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala
Ndg. Simon Berege, mratibu wa program ya Afya ya kinywa na meno Ndg. Christian Noah amesema msaada huo utasambazwa katika shule za Msingi
za kata zote za Halmashauri ya Msalala ili walimu waweze kufundisha kwa vitendo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Simon Berege aliipongeza Kampuni ya Colgate Palmolive kwa kutoa elimu yenye manufaa
kwa jamii kwa kuwa elimu hii inatolewa kwa watoto ambao ni dhahiri kuwa wataendelea kuieneza elimu hiyo mpaka umri wa uzeeni kwao na kuiomba
Kampuni hiyo zoezi hili liwe endelevu. Mkurugenzi Mtendaji huyo aliendelea kuwataka wadau wengine kujitokeza na kuiga mfano mzuri ulioneshwa
na Kampuni ya CoLgate Palmolive na kuahidi kutoa ushirikiano.
Kampuni ya Colgate Palmolive East Africa LTD imeendesha Mafunzo kwa walimu 25 wa shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Mafunzo hayo yametolewa na ndg. Christian Noah mratibu wa program ya Afya ya kinywa na meno Tanzania. Ndg. Christian Noah amesema Kampuni
ya Colgate Palmolive itaendelea kutoa elimu hii kwa vitendo kila mwaka na kusisitiza kuwa maeneo yote ya Halmashauri yatafikiwa. Mafunzo hayo
yamelenga wanafunzi wote wa shule za Msingi Tanzania na watakaopatiwa miswaki na dawa ya Colgate ni watoto wenye umri wa miaka 5-9.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.