KATIBU TAWALA MKOA WA SHINYANGA AWAASA KAMATI YA UJENZI KITUO CHA AFYA CHELAA
Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Ndg. Albert Msovela akifuatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Ndg. Rashid Mfaume na kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Chela kilichopo katika Halmashauri ya Msalala na kuzungumza na kamati za mapokezi na ujenzi. Akizungumza mbele ya kamati hizo Katibu Tawala huyo aliwataka kuongeza kasi ya usimamizi wa ujenzi kwani ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi wa tano sambamba na hilo Ndg. Msovelo aliwataka waanakamati na Uongozi wa kituo cha afya Chela kubainisha mipaka ya kituo hicho ili kuepusha wanchi wa maeneo jirani kuvamia maeneo ya kituo hicho. Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala alimhakikishia Katibu Tawala huyo kuwa ujenzi wa kituo hicho utakwenda kwa kasi na kwa ubora unao kidhi vigezo kwani wamekwisha jipanga. Pia Ndg. Msovela alizungukia mipaka ya eneo la kituo cha afya hicho na kujiridha na ukubwa wa eneo lililotengwa kwa ajili ya kituo hicho.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.