KIKAO CHA WADAU WA ELIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA
Kikao cha wadau wa elimu kilicho fanyika tarehe 21/08/2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya Msalala na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari , Waratibu elimu kata wote , Watendaji wa kata , Mkuu wa Wilaya , Hakimu pamoja na viongozi mbalimbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Kikao hicho kilifanyika kwa lengo la kutathimini na kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili wanafunzi hususani mototo wa kike pamoja na kujadiliana kwa pamoja namna ya kuzitatua changamoto hizo.
Changamoto zilizo jadiliwa ni pamoja na Utoro , Umbali wa makazi na shule , Mimba kwa motto wa kike ,
Baada ya kujadiliana kwa pamoja changamoto hizo waliweka mikakati ya pamoja ikiwa ni pamoja na kwenda kuhamasisha ujenzi wa hosteli ( ujenzi wa mabweni ) kwa shule za Sekondari , Kutoa elimu ya kujitambua kwa mototo wa kike , kila shule iwe na mwalimu wa kike , kuwapima watoto wa kike mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu na kutoruhusu wanafunzi kutembea mmojammoja na hivyo kuwa shauli watoto wa kike watembee waili au zaidi .
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.