KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ATOWA WITO KWA WAZAZI
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho ametowa wito kwa wazazi juu ya uwajibikaji katika swaala la elimu ambapo amewa waasa wazazi kuchangia chakula mashuleni ili watoto wao waweze kupata angalau mlo mmoja kwa siku kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza tatizo la utoro mashuleni pia aliwataka wazazi waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwanunulia watoto wao mahitaji muhimu ya shule kama viatu madaftari nk. Kiongozi huyo wa mbio za mwenge alizungumza hayo leo tarehe 22.08.2018 alipotembelea kituo cha Afya Mhandukilichopo katika kata ya Chela ambapo alikwenda kujione shughuli za tohara kwa wanaume .
Kwa upande mwingine Ndg. Charles Francis Kabeho alitowa wito kwa wananchi juu ya faida inayopatikana kutokana na kufanyiwa tohara kwani kwa mtu aliyefanyowa tohara inapunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya ukimwi pia kiongozi huyo aligawa vitabu kwa viongozi wa Vijiji ili viweze kuwasaidia katika uelimashaji kwa jamii juu ya faida zitokanazo na mtu kufanyiwa tohara.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.