Hiyo ni kauli iliyotolewa leo na kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango iliyokuwa inaongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala MHE. Mibako Mabubu wakati wa kikao hicho cha mwisho wa mwezi wa Disemba, ambapo wajumbe wa kikao hicho kwa kauli moja wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji (W) na wataalamu kuongeza jitihada katika kukusanya mapato ya Halmashauri kwani ndiyo yanayoiwezesha Halmashauri kuendesha shughuli zake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji (W) ndugu Simon Berege amepokea ushauri huo na kuwaomba waheshimiwa madiwani kumpa ushirikiano pindi atakapokuwa kwenye utekelezaji wa agizo hilo kwani aliwawezesha baadhi ya wajumbe wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kufanya ziara kwenye maeneo mengine ya nje ya Halmashauri ya Msalala ili kuweza kujenga uelewa wa pamoja na hivyo Waheshimiwa Madiwani wawe mabalozi kwenye maeneo yao ya utendaji.
Halmashauri ya Msalala mapato yake makubwa ilikuwa inategemea Mgodi wa madini ya dhahabu wa Bulyanhulu uliyopo kata ya Bulyanhulu, ambapo mgodi huo ulichangia 75% ya mapato ya Halmashauri na 25% iliyobaki ilipatikana kupitia makampuni madogo madogo yanayofanya kazi na mgodi huo, minada ya ng’ombe, magulio, leseni ya biashara, nyumba za kulala wageni, wachimbaji wadogo wadogo, ushuru wa mazao hasa dengu, mpunga na matunda na ushuru wa stendi ya Bugarama. Hivyo mgodi uliposimamisha shughuli zake Halmashauri hii iliathirika sana kimapato.
Juhudi za kuondokana na hali hii zimefanyika ambapo timu ya wataalamu wa Halmashauri hii ikishirikiana na waheshimiwa Madiwani na MHE. Mbunge Ezekiel Maige wameandaa maandiko ya miradi mbalimbali mfano mzuri ni upanuzi wa eneo la kulaza magari na Stendi Isaka, ujenzi wa uzio kwenye minada, hii ni baadhi ya mipango ambayo ikikamilika tunategemea Halmashauri itaboresha mapato yake sambamba na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) kusimamia ipasavyo ukusanyaji huu wa mapato. Rai kwa wananchi ni kuhakikisha tunalipa kodi mbalimbali na tozo zote kwa hiari kwani kufanya hivyo tutamunga mkono jitihada za Rais wetu mpendwa MHE. Rais JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI za kuwaletea wananchi wetu maendeleo.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
MSALALA
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.