Kauli hii imetolewa leo na waziri wa madini MHE. Doto Biseko wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha kakola ndani ya Halmashauri ya Msalala
wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Katika mkutano huu viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo Katibu Tawala ndg. Simon Ndanya ambaye alimuwakirisha
Mkuu wa Wilaya, Meneja wa mamlaka ya madini mkoa wa Shinyanga, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Msalala ndg. Simon Berege, vyombo vya ulinzi na usalama,
Wakuu wa idara na vitengo na wananchi. Mkutano huo uliwahusu wachimbaji wadogo wadogo ambapo Mhe. Biteko aliwataka wachimbaji hao kulipa kodi ya Serikali.
Waziri huyo amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali zao ambazo Mwenyezi Mungu amewajalia hivyo kutoa rai
kwa watanzania wote hususani wanaojihusisha na biashara ya madini kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima na Serikali kwa kuhakikisha wanalipa kodi kwa madini wanayonunua
na kuepuka kusafirisha nje ya nchi madini hayo pasipo kulipa ushuru wa Serikali kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma jitihada zinazofanywa na MHE. Rais John Pombe Magufuli
za kuwaletea wananchi maendeleo. Unapolipa kodi barabara, hospitali, shule zitajengwa pamoja na upatikanaji wa huduma bora za maji na umeme kwani maendeleo yetu yataletwa
na watanzania wenyewe hivyo tulipe kodi.
Hatua mbalimbali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaokamatwa kutorosha madini pasipo kulipia kodi ya Serikali, miongoni ya adhabu hizo ni kutaifishwa kwa madini yatakayokamatwa na kufirisiwa kwa mali zake zote hivyo nawaomba wana kakola kujiepusha na biashara haramu kwani imeshakuwa zilipendwa. MHE. Biseko ametoa mifano wa watu wanaofanya
biashara za dhahabu pasipo kulipa kodi ya Serikali katika eneo hilo la kakola na kusema tayari wafanyabiashara hao wamekamatwa hivyo kuwataka wachimbaji wadogo wadogo kuuza dhahabu zao
kwenye masoko ya Dhahabu yanayotambuliwa na Serikali ili kuwezesha Serikali kupata mapato na hivyo kuunga mkono jitihada za Rais wetu.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.