Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba wakati wa kikao cha lishe cha ngazi ya kata kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Msalala uliopo
katika Kata ya Ntobo.Mkurugenzi huyo amewapongeza Watendaji wa Kata kwa usimamizi mzuri wa lishe katika kata zao kwani matokeo ya green kadi yanaonyesha hali ya lishe katika
Halmashauri yetu ipo vizuri,hii imetokana na kujengea uwezo wananchi kupitia elimu.Hongereni kwa usimamizi mzuri wa lishe katika Kata zenu,niombe shule zinazotoa chakula kwa
madarasa ya mitihani pekee zihamasishe jamii ili ichangie chakula cha kutosheleza wanafunzi wa shule nzima.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi wa kikao hicho,Daktari wa Halmashauri ya Msalala DR.Sisti Mosha amesema jamii kwa kiasi kikubwa imehamasika na tatizo la utapiamlo kwa watoto
limepungua katika robo hii ya nne,haya ni mafanikio makubwa kwa halmashauri yetu mimi pamoja na watumishi wengine wa idara za afya,elimu,kilimo,mipango na wadau mbalimbali
tutaendelea kuelimisha jamii na kufanya suala la lishe kuwa kipaumbele cha kwanza katika shughuli zetu za kila siku kwani lishe bora huwezesha mtu kuwa na upeo mkubwa wa kufanya
maamuzi katika masuala mbalimbali ya maisha.
Akiwasilisha taarifa ya lishe ndani ya Halmashauri ya Msalala, Mratibu wa lishe Bwana Peter Nganzo amesema katika robo ya nne inayoanzia Aprili hadi Juni kumekuwa na ongezeko
au mwamko mkubwa hasa kwa kinamama wajawazito kuhudhuria kliniki na kupima afya zao.Kwa kipindi cha miezi mitatu taarifa zinaonyesha watoto 3626 walizaliwa huku watoto waliozaliwa
wakiwa na uzito pungufu ya kilo 2.5 wakiwa 69 sawa na 1.9% ya watoto wote waliozaliwa.Sambamba na hilo shule 113 za msingi na shule za sekondari 24 zinatoa chakula kwa wanafunzi
wake.Tuendeleze mapambano ya udumavu kwa pamoja kwa kula milo yenye makundi sita ya chakula ambayo ni protin,wanga,mbogamboga,mafuta,matunda na sukari.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.