Huduma ya lishe katika halmashauri ya msalala inaendelea kutolewa na kuwasaidia watoto wenye utapiamlo, mwenyekiti wa lishe ndug; Mwamini Mziray ametoa PD report (Postive Deviants) leo tarehe 09/11/2018 iliyo fanyika katika kijiji cha Runguya chenye vitongoji vitatu, ambapo walipima watoto 210 nakukuta nusu ya watoto hao wana utapiamlo. Mwenyekiti ameendelea kusema kuwa wakimaliza kupima wale watoto ambao watagundulika kuwa wana utapiamlo huwaandalia darasa na kuwapikia vyakula vyenye lishe ili kuwasaidia kuepukana na hali hiyo ya utapiamlo.
Pia HTS (HIV Testing and Canceling) wameeleza jinsi walivyo boresha mpango wao wa HTS kwamba mtu yeyote ambaye ataenda kuangalia afya yake (mteja) akikutwa na virusi vya ukimwi ataombwa kutaja na wenzi wake ambapo wao watafatilia hao watu walio tajwa na kuwapima ili na wao kuchunguza afya zao, pia wamesema kuwa mteja wao atapimwa mra mbili wakimaanisha mda huo alio gundulika na mda ambao atahitajika kupewa huduma ya dawa ili kuhakikisha kuwa ana virusi vya ukimwi kweli. Alimaliza kwa kusema kuwa wanawaomba watu kwenda kuzifanyia uchunguzi afya zao (kupima).
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.