Fedha zinazotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hasain zimeendelea kuinufaisha Halmashauri ya Msalala kupitia kukamilisha vyumba vya madarasa 90 na Kituo cha Afya cha Tarafa ya Isagehe ambacho kinajengwa ndani ya Halmashauri hiyo katika Kata ya Mwalugulu. Maelezo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama ndugu Festo Kiswaga wakati wa ziara ya kamati ya Siasa Mkoa.
Ziara hiyo imeongozwa na mwenyekiti wa CCM Mhe. Mlolwa akiambatana na wajumbe wa kamati hiyo, Kamati ya Siasa Wilaya ikiongozwa na Mhe. Thomas Myonga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Mibako Mabubu, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Msalala na wataalamu wa Halmashauri hiyo.
Lengo la Ziara hiyo ni kukagua Miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ikiwemo Ujenzi wa vyumba vya Madarasa 4 vikiwa na viti na meza zake vilivyogharimu Tsh. 80,000,000/= fedha zilizotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huu sHalmashauri kwa kutumia vizuri fedha zilizotolewa na kuwaomba wananchi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanafanya hivyo.
Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Isagehe una majengo 3 ambayo ni OPD, Maabara na kichomea taka ambao utagharimu Tsh. 250,000,000 fedha za tozo za miamala za simu ambazo zimetolewa na Mhe. Mama Samia Suluhu Hasain sambamba na ujenzi wa uzio wa mnada wa Bulige ambao Halmashauri imetenga Tsh. 150,000,000/= kutoka mapato ya ndani ambapo kamati imeshauri spidi ya ujenzi kuongezwa ili miradi ianze kutumika kwani ni ahadi za Serikali kutoa huduma za uhakika za Afya na ukusanyaji mapato.
Kamati hiyo ilitembelea pia kikundi cha Upendo kinachoongozwa na kina mama ambao wanajishughulisha na utunzaji wa mpunga kwenye ghala la mazao, ambapo wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kuwaendeleza kinamama kwani kwa sasa wanahifadhi mazao hadi bei inapopanda ndipo huuza kwa bei nzuri na hivyo kuwezesha kufanya marejesho ya mkopo waliochukua. Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM (M) ameitaka Halmashauri kukiongeza mkopo kikudi hicho ili kuweze kununua mashine ya kisasa ya kukoboa mpunga na kuugrade, suala ambalo Mkurugenzi Mtendaji (W) ameridhia na kusema atawakopesha Tsh. 60,000,000 kwa kuwa mkopo wa mwanzo Tsh. 38,000,000 tayari wameshamaliza deni lao.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.