Kauli hii imetolewa leo na wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango iliyoongozwa na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Msalala Mhe.Mibako mabubu wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea miradi ya
maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri.
Ziara hiyo imepitia miradi sita katika kata mbalimbali zikiwemo ukamilishaji wa jengo la zahanati ya
mwashigini na ujenzi wa vyumba 2 vya maabara katika shule ya sekondari Mwakata kata ya Mwakata.
Ukamilishaji wa bweni la wavulana katika shule ya Sekondari isaka na ujenzi wa bwalo la chakula katika
kata ya Isaka. ujenzi wa jengo la upasuaji, wodi ya wanaume na watoto, jengo la mionzi na jengo la
kufulia katika Hospitali ya Halmashauri iliyopo kata ya Ntobo. Miradi mingine iliyotembelewa ni ujenzi
wa Kituo cha Afya segese ambacho kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri. pamoja na
ujenzi wa zahanati ya Nyamishiga ambayo inajengwa na wananchi wa kijiji hicho wakishirikiana na wachimba
madini wa eneo hilo.
Miradi yote niliyoitaja inagharimu Tsh. 1,241,000,000 kutoka Serikali kuu na Fedha za mapato ya Ndani ya
Halmashauri. Miradi yote ipo katika hatua nzuri za umaliziaji na kamati imesisitiza miradi hiyo ikamilike
ndani ya mwaka wa fedha huu kwani fedha ipo hivyo mafundi waongeze kasi ya ujenzi.
Sambamba na ziara hiyo, wajumbe hao pia wamefahamishwa uwepo wa vifaa vya kisasa vya kutolea huduma katika
Hospitali ya Halmashauri na kuombwa kuwa mabalozi kwa wananchi kwani Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Samia Suluhu ametoa vifaa hivyo kwa Hospitali za wilaya nchini ili kusogeza huduma karibu
na wananchi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.