MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE HALMASHAURI YA MSALALA 2017-07-17
Tarehe 13-07-2017 mwenge wa uhuru ulipokelewa katika halmashauri ya Wilaya ya Msalala katika kata ya Bulige muda wa saa 3:00 asubuhi na viongozi wa Halmashauri ya msalala, Wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Ndg.Fadhiri Nkurlu, na Mkurugenzi wa Halmashari ya Msalala Ndg. Simon Berege
Miradi iliyo zinduliwa katika katika halmashauri ya msalala
Jumla ya miradi 10 iliyo kamilika na kuzinduliwa na mbio za mwenge katika halimashauri ya Msalala ilikuwa na jumla ya thamani ya shilingi 1,528,09300429.00
Baada ya mwenge kupokelewa katika kata ya bulige ulianza kuzindua baadhi ya miradi , ikiwemo uzinduzi wa soko na Ghala la kuhifadhi nafaka na kuwekewa jiwe la msingi na Ndg.Amour Hamad Amour.
Baada ya kuzindua mradi katika kata ya Bulige mwenge ulielekea katika kata ya Ngaya na kupokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa kata ya Ngaya , katika kata ya Ngaya baadhi ya miradi ilizinduliwa ikiwemo uzinduzi wa mradi wa maji na barabara ya kutoka kata ya Ngaya kwenda kata ya Busangi.
Baada ya mwenge wa uhuru kutoka kata ya Ngaya ulielekea katika kata ya Chela na mara baada ya kufika kulitolewa ujumbe wa mwenge uliohusu kulinda raslimali za taifa letu hasa madini ili yaweze kulinufaisha taifa na wananchi wake piakujilinda na magonjwa ya ukimwi na Maleria.
Baada ya kutolewa ujumbe wa mwenge, mwenge wa uhuru ulielekea shule ya sekondari Baloha na kupokelewa na wananchi pamoja na wanafunzi kwa shangwe na nderemo . Kiongozi wa mbio za mwenge alisomewa risala na wanachama wa klabu ya wapinga rushwa katika shule hiyo, na mara baada ya kusomwa kwa ujumbe huo kiongozi wa mbio za mwenge Ndg.Amour Hamad Amour aliwakabidhi wanafunzi hao cheti cha TAKUKURU.
Mara baada ya mwenge wa uhuru kutoka shule ya Sekondari Baloha ulielekea katika zahanati ya Mhandu ambapo ulizindua mradi wa zahanati na baadae kuelekea makao makuu ya halmashauli ya Wilaya ya msalala katika kata ya Ntobo ambapo msafara ulijionea shughuli za vijana hususani eneo itakapojengwa ofisi za vijana, ambapo vijana walikopeshwa mashine za kufyatulia matofali.
Baada ya tukio hilo mwenge wa uhuru ulielekea katika kata ya Segese ambako ndipo mwenge wa uhuru ulikesha , katika kata hii pia mwenge wa uhuru ulipokelewa na wananchi wa maeneo yote ya kata ya Segese kwa shangwe kubwa na vigeregere , nderemo na vifijo .Mara tu mwenge wa uhuru ulipofika segese kiongozi wa mbio za mwenge alizindua vyumba vitatu vya madarasa na kuweka jiwe la msingi ,na kuzindua mradi wa kiwanda cha mafuta ya alizeti katika kata hiyo.
Mwenge wa uhuru ulipo wasili katika viwanja vya shule ya msingi Segese kiongozi wa mbio za mwenge aliangalia maendeleo ya uwajibikaji wa shughuli za kujenga taifa kwa vijana wa kata ya Segese.Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru 2017-07-17. Mwenge wa uhuru ulibeba kauli mbiu isemayo SHIRIKI KUKUZA VIWANDA KWA MAENDEREO YA NCHI YETU .Pia Tanzania bila ukimwi na madawa ya kulevya inawezekana kwa kuzingatia hayo zoezi la upimaji wa VVU liliendelea ambapo zaidi ya watu 436 walijitokeza kupima na kati ya hao wote ni watu 16 pekee walio patikana na maambukizo. Na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya magunia zaidi ya magunia 10 ya bangi yalikamatwa na kuteketezwa kwa moto , mwenge oyee .
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.