Umati mkubwa wa wananchi wa Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama leo tarehe 13/08/2024 umejitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2024 katika
Kijiji cha Bulige, kata ya Bulige ambapo mapokezi hayo yamepambwa na vikundi mbalimbali vya burudani za asili na wasanii wapya wa kizazi kipya ambao
wamekesha hapo kwa ajili ya kuutendea haki Mwenge huo wa Uhuru.
Awali Akipokea Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala (W) ya Kahama NDG. Hamad Mbega toka kwa Katibu Tawala (W) ya Shinyanga Vijijini amesema Mwenge wa Uhuru
utakimbizwa katika kata za Bulige,Ngaya na kupitia kata za Busangi na Ntobo na baadae kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Masabi kata ya Mega na kuma
lizia miradi 4 katika kata ya Segese.
Mbio za mwenge wa Uhuru 2024 zimebeba ujumbe wa "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu.Nae kiongozi wa mbio
za Mwenge wa uhuru kitaifa NDG.Godfrey Eliakimu Mnzava ameitaka jamii kutunza mazingira kwa manufaa ya vijazi vijavyo sambamba na kushiriki kwenye uchaguzi
wa Serikali za mitaa ili kuwezesha kupata viongozi wawajibikaji.
Kwa upande wa Mbunge wa Msalala, MHE.Idd Kassimu Idd amepongeza Jitihada za Dkt. Samia kwa kuwezesha Halmashauri kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kama
mbio za mwenge 2024 zitakavyoshuhudia.Mbio za mwenge wa Uhuru 2024 zimepitia miradi 9 yenye thamani ya Tshs.460,497,725.42 ambapo mradi wa ujenzi wa bweni la
watoto wenye mahitaji maalum umetolewa maelekezo ya kufanyiwa marekebisho na baada ya marekebisho mradi ufunguliwe. Miradi 8 imekaguliwa na kupitishwa.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.