Siku ya wakulima (Farmer Field Day) imefanyika leo tarehe 09, sepemba 2021 katika Kata ya Segese, Halmashauri ya Msalala chini ya
usimamizi wa shirika la TAHA,na Halmashauri ya Msalala pamoja na na kuhudhuliwa na wafadhiri ambao ni Serikali ya watu wa Korea
(KOICA,) UN&WOMEN, UNFPA , Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Festo Kiswaga , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg
Charles Edward Fussi, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Ushetu Pamoja na wataarau toka halmashauri ya Msalala, Ushetu na Kahama
Manispaa.
Katika Hafla hiyo Mgeni rasimi Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Festo kiswaga na wageni waalikwa walipata fulsa ya kutembelea na
kukagua shughuli mbalimbali za kilimo zinazofanywa na wanakikundi cha LUMOLUMO chini ya usimamizi wa Shirika la TAHA kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Msalala chini ya ufadhiri wa Serikali ya watu wa Korea (KOICA,) UN&WOMEN pamoja na UNFPA.
Katika maadhimisho hayo Ndg Festo Kiswaga alilidhishwa na shughuli zinazofanywa na kikundi hicho na kuwaomba wadau wa
UN&WOMEN pamoja na shirika la KOICAkuona sasa kunahaja ya kuongoze maeneo ya mradi ili kuwasaidia wanchi kuongeza kipato na
kupunguza utegemezi kwa akinamama na vijana kwa kwa kufanya hivyo kutawajengea uwezo wa kujitegemea. Pia aliwaomba watu wa
mgodi wa BARICK Bulyanhulu kuwasaidia wakulima hao kwa kununu mazao yao kwani yanaubora wa kiwango cha hali ya juu.
Sambaba na hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Charles Edward Fussi aliwaahidi wanakikundi hao kuwa
Halmashauri ya Msalala itashirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha wanapata mafanikio kwa kuwapatia Mikopo. Pia aliwataka wanachi
wakawe mabalozi wazuri kwa kuiga ba kueneza shughuli/ utaalamu walio jifunza kupitia shamba darasa linalomilikiwa na kikundi cha
LUMOLUMO kwa lengo lakuongeza tija zaidi.
Mashamba darasa haya pia yanafanyika katika maeneo mengine ndani ya Halmashauri ya Msalala ambayo ni Shilela na Lunguya.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.