Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Christina Mndeme leo amekagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa kituo
cha Afya Bulige,ambapo jumla ya majengo 6 yatajengwa.Majengo yaliyokamilika mpaka sasa ni Jengo la mama na mtoto,jengo
la upasuaji,jengo la maabara na jengo la wagonjwa wa nje na kubakiza majengo mawili ya wodi ya mama na watoto na nyumba
ya mganga mfawidhi.Mradi huo hadi kukamilika utatumia Tsh.Milioni mia tano,fedha ambazo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr.Samia Hasain Suluhu kuhakikisha afya za watanzania zinalindwa.
Mkuu wa Mkoa huyo ameridhishwa na hatua zilizofikiwa na kuitaka Halmashauri kukamilisha mapema ili huduma za afya zianze
kutolewa na amempongeza Rais Samia Suluhu kwa kuwathamini wananchi wa kipato cha chini kwani uwepo wa kituo hiki kitapunguza
gharama za kusafiri kufuata huduma sambamba na kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji mali kwani kimeokoa muda.
Awali akisoma taarifa ya kituo hicho mganga mfawidhi,Dr.Kihoza amesema kituo hicho kitahudumia zaidi ya watu 39400 kwani Bulige
imezungukwa na wachimbaji wa madini toka Halmashauri ya Shinyanga vijijini na hupata huduma Bulige.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Mhe.Mibako Mabubu amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kumfikishia shukrani
Rais Samia Suluhu kwa kuitengea fedha halmashauri kiasi cha bilioni 7 kwa mwaka 2023-24 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
ndani ya halmashauri na kuahidi kukamilisha miradi hiyo kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati ili kuunga mkono matarajio ya serikali
ya awamu ya sita.Nae Mwenyekiti wa CCM(W) Mhe.Thomas Myonga amewataka wananchi wa kata ya Bulige na Watanzania kwa ujumla kutopotoshwa
na wanasiasa wanaotaka madaraka pasipo matendo kwani Serikali inayoongozwa na CCM inatekeleza vizuri ilani yake kwa kusikiliza kero
za wananchi na kuzitatua hivyo kwa pamoja tumuunge mkono Rais wetu kwa kufanya kazi kwa bidii.
Katika Mkutano wa hadhara,Mkuu wa mkoa ametoa nafasi kwa wananchi kuuliza maswali au kuelezea changamoto zinazowakabili wananchi wa
kata ya Bulige ambapo wananchi wengi wamejitokeza na kuelezea changamoto walizonazo, baadhi ya changamoto zilizowasilishwa ni pamoja
na uwepo wa kusuasua kwa umeme suala ambalo mratibu wa umeme vijijini(REA) amelitolea ufafanuzi kuwa inatokana na maboresho yanayofanywa
na Tanesco kuongeza uzalishaji wa umeme nchini,katika suala hili Mkuu wa Mkoa ameitaka Tanesco kutoa ratiba kwa wananchi ili wafahamu
mda umeme utakuwepo au kutokuwepo.Suala lingine lililoulizwa ni uwepo wa fedha 10% kwa wanawake na vijana pia huduma ya mfuko wa afya
ya jamii(CHF).Changamoto hizi zimetolewa ufafanuzi na Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba ambapo amesema fedha ya 10% ni mkopo
usiokuwa na riba unaotolewa kuwezesha wanawake,vijana na walemavu kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali na baada ya mda kurejesha,takwimu
zinaonyesha watu wengi hawarejeshi hivyo kuomba walionufaika kurejesha fedha hizo kwa wakati ili wengine wakopeshwe.CHF ni bima inayowezesha
kaya kupata huduma za afya kwa kaya kuanzia mtu mmoja na ukomo wake watu sita kwa kipindi cha mwaka mmoja,hivyo jamii jiungeni kurahisha
matibabu.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.