Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Tellack amezitaka Halmashauri za mkoa wa Shinyanga kuepuka hoja za ukaguzi zisizokuwa na mashiko kwani hoja nyingi zipo ndani ya uwezo wa Halmashauri kuzizuia na hivyo kuwezesha mkoa kuwa na hoja chache. Maneno hayo ameyasema Mkuu wa mkoa huyo leo katika kikao cha baraza la madiwani cha kupitia hoja za ukaguzi za 2017/18 katika Halmashauri ya Msalala ambapo kikao hicho kimehudhuliwa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Katibu Tawala (M) ndugu Albert Msovela, Mkuu wa Wilaya ya Kahama ndugu. Anamringi Macha, Mhe. Ezekiel Maige Mbunge jimbo la Msalala, Mhe. Mibako Mabubu mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi wa Halmashauri ndugu. Simon Berege, vyombo vya ulinzi na usalama mkoa na wilaya, wah. Madiwani na wataalamu.
Awali akimkaribisha Mkoa wa Mkoa , MHE. Mibako Mabubu Mwenyekiti wa kikao hicho amemshukuru mkuu wa mkoa na timu yake kwa kukubali kuja kuhudhulia kikao hicho na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo yote ya serikali yatakayotolewa. Katika salamu zake MHE. Ezekiel Maige (MB) amemhakikishia mkoa wa mkoa huyo kuwa katika Halmashauri ya Msalala kuna ushirikiano mzuri kati ya watumishi wa serikali na WAH. Madiwani na hivyo kurahisisha utekelezaji wa sera za chama Tawala. Kwa upande wake Katibu tawala (M) ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha inasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato pia matumizi yake sambamba na kuomba watumishi wasiondolewe kwenye mfumo wa mishahara hadi watakapopata taarifa toka mkoani.
Katika kikao hicho hoja mbalimbali zilijadiliwa na kutolewa majibu na ufafanuzi ambapo mweka Hazina wa Halmashauri hiyo ndugu. Masatu Mnyoro katika utangulizi wake alisema Halmashauri ya Msalala tangu ianze kazi rasmi ( 2013) imepata hati safi mara 4 na hati yenye mashaka mara 1 mwaka 2016/17, na kuendelea kusema katika 2017/18 Halmashauri imepata hati safi hii yote imetokana na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi Mtendaji ndugu. Simon Berege na baraza la WAH. Madiwani. Kimsingi katika 2017/18 hoja nyingi zimetokana na kushuka kwa mapato ya Halmashauri ambayo imetokana na kushuka kwa uzalishaji wa madini kwa kampuni ya ACCACIA kwani mapato ya Halmashauri yalitegemea uzalishaji wa madini kwa 85% na hivyo kuahidi hoja nyingi kufungwa mara baada ya kulipwa deni linaloidai kampuni ya Accacia sambamba na kuahidi kuzifuta hoja zingine ambazo zilikosa viambata kwani kwa sasa viambata hivyo vimepatikana.
Nae Mkaguzi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga (CEA) ameitaka Halmashauri kuwasilisha majibu ya hoja mapema ili ofisi yake iweze kupitia na kuona kama majibu yanakidhi haja ya ufungaji hoja hizo na kuomba Halmashauri kuwatumia wakaguzi wa ndani na ofisi yake kusaidia ufafanuzi wa hoja hizo ili zifungwe.
Imetolewa na Kitengo cha TEHAMA Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.