Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe.Mboni Mhita amepongeza jitihada zinazofanywa na viongozi wa Halmashauri ya Msalala kwa kuthamini
na kuunga mkono Jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu,kwani Halmashauri hiyo imepokea
fedha nyingi kutoka kwa Mhe. Rais mama Samia Suluhu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata na vijiji mbalimbali.
"nani kama Rais mama Samia Suluhu" na halmashauri ili kuendana na kasi ya Mhe.Rais leo imejiongeza kwa kuwajengea uwezo waheshimiwa
Madiwani wote na wakuu wa Idara na Vitengo wote ili waweze kusimamia na kutekeleza vema ilani ya Chama cha Mapinduzi kwani CCM ndio
wenye thamana ya kuwaletea maendeleo Watanzania, hongera sana Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji(W) kwa kuonyesha njia
kuelekea maendeleo.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mibako Mabubu amesema," tunaridhika na maendeleo yanayofanywa na
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu kwani tangu Halmashauri ianzishwe mwaka 2013 haijapata kutokea fedha
za maendeleo kuletwa kwa wingi kama inavyofanya Serikali ya awamu ya sita,tunaomba tufikishie salamu zetu kwa Mhe.Rais Samia Suluhu.
Sisi kama viongozi wa Halmashauri ya Msalala tunazisimamia vema fedha hizo na ndio maana leo hii tumeona vizuri tukumbushane majukumu
yetu kwa kuwaomba wataalamu toka ofisi ya Katibu Tawala kuja kutupatia Mafunzo ya mpango wa bajeti,lengo likiwa ni tuweze kutekeleza
vizuri ilani ya Serikali iliyotuweka Madarakani.
Nae Katibu wa Chama cha Mapinduzi amewataka viongozi hao kupokea kero za wananchi kila wakati na kuzipatia ufumbuzi ili kuweza kutekeleza
matarajio ya wananchi kama tulivyowaahidi sasa ni lazima tutekeleze,Serikali ya awamu ya sita ni sikivu hivyo leteni kero za wananchi na
kwa pamoja tushirikiane kuzitafutia utatuzi lengo likiwa ni kuleta maendeleo kwa jamii zetu.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa, amesema taasisi yake imejipanga kufanya ukaguzi wa miradi yote inayotekelezwa
ndani ya Halmashauri sambamba na kutoa elimu ya huduma ya Takukuru rafiki kwa wananchi ili kuongeza uwajibikaji wa watumishi kwa wananchi wanaowa
ngoza na hivyo kuomba ushirikiano pindi watumishi wa taasisi hiyo wanapotembelea vitongoji,kijiji au kata zao.
Nae Katibu Tawala (W) ya Kahama ndg.Mohamed Mbega amewaomba viongozi hao kufuata Sheria,taratibu na Kanuni katika utekelezaji wa majukumu ya kila
siku ili kuondoa matatizo yasiyokuwa ya lazima na kuahidi kutoa ushirikiano muda wowote atakapohitajika.Wakufunzi wa Mafunzo hayo wameipongeza
Halmashauri kwa kuona umuhimu wa kujengeana uwezo kwani elimu ndio msingi wa maendeleo, miongoni mwa mada zinazofundishwa katika mafunzo haya ni
maandalizi ya mpango wa bajeti,maadili ya uongozi na utumishi wa umma, Dhana ya uzalendo kwa Serikali, Mahusiano ya Halmashauri na Serikali kuu
na miundo na majukumu ya kamati za kudumu za Halmashauri.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.