MKUU WA WILAYA KAHAMA ATAKA ELIMU IZINGATIWE
Mkuu wa Wilaya ya Kahama ndugu. Anamringi Macha ameitaka jamii ya wakazi wa Halmashauri
ya Msalala kuwekeza kwenye elimu kwa watoto wao kwani Serikali ya awamu ya tano ni Serikali
inayohitaji kila mwanajamii mwenye mtoto aliyefikisha umri wa kwenda shule apelekwe kwa kuwa
elimu inatolewa bure, kinachotakiwa ni mzazi kuweza kumwezesha mtoto kuhudhuria masomo
kwa kumnunulia sare za shule, viatu, madaftari na kalamu. Amesisitiza kuwa wazazi watimize wajibu
wao wa kutimiza mahitaji ya muhimu kwa watoto wao nae yupo tayari kushirikiana na viongozi kuhaki
kisha kila mzazi anatimiza wajibu huo. Maelezo haya yametolewa leo katika kikao cha kumaliza robo ya nne ya mwaka 2017/18 cha baraza la madiwani kilichofanyika makao makuu ya Halmashauri ya Msalala
iliyoko kata ya Ntobo.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya huyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Mibako
mabubu amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanamsalala
wanapata maendeleo kwani ameshiriki katika ziara mbalimbali za kimaendeleo zilizofanyika katika
Halmashauri ya Msalala na kumwomba aendelee na jitihada hizo.
Ndugu Macha amewataka waheshimiwa madiwani kuwatumikia wananchi kama ilani ya chama cha
Mapinduzi inavyotaka kwa kuwa wananchi tayari walishamaliza kazi yao kwa kuwachagulia mafiga
matatu kama walivyoomba hivyo ni jukumu la Madiwani sasa kuhakikisha miradi inayofanyika katika
maeneo yao wanaisimamia na kuhakikisha inakamilishwa kwa ubora sambamba na kuanza kutumika
ili wananchi waone matunda ya Serikali yao, alitoa wito kwa jamii kuitunza miradi hiyo. Mwisho Mkuu
wa Wilaya huyo aliwataka watumishi kuhamia Ntobo ili waweze kufanya kazi kwa ufasaha nay eye
amesema atatenga siku za kufanya kazi katika Halmashauri zote 3 na kumwomba Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Msalala kumpatia Ofisi ili aweze kutatua changamoto za Wakazi wa Msalala kwa
Ukaribu sambamba na kutembelea miradi ya maendeleo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.