Kauli hii imetolewa na Kiongozi wa Mwenge Kitaifa Ndg.Abdalla Shaib Kaim alipokuwa akihutubia wananchi wa Halmashauri ya Msalala katika kijiji cha kakola ambapo mwenge wa uhuru utakesha
na tarehe 02-08-2023 kukabidhiwa Halmashauri ya Nyagwale mkoani Geita.Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo kutokana na kuridhishwa na miradi iliyotekelezwa ndani ya Halmashauri kwani miradi
yote ni mizuri,imejengwa kwa viwango vya juu sambamba na miradi hiyo kuwa na nyaraka zote za ujenzi, hongera sana watumishi mnaitendea haki Serikali ya awamu ya sita kwa kufanya kazi kwa
weledi,endeleeni kuwatumikia Watanzania kwa moyo huu wa kuthamini mali za Serikali na kuzisimamia.
Kiongozi huyo ameitaka jamii kuhakikisha inapinga mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa sehemu stahiki,kujikinga na ugonjwa wa Maleria na ukimwi sambamba na kuunga mkono mapambano
dhidi ya madawa ya kulevya pia jamii izingatie lishe kwa afya njema,jamii itumie zaidi matunda na mbogamboga na kupunguza na matumizi ya vyakula vya wanga na sukari sanjali na kufanya
mazoezi walau nusu saa kila siku.
Ndg.Abdalla Shaim Kaim amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya Msalala kwa kuwa wazalendo kwani mahali pote mwenge ulipopita wananchi wamejitokeza kwa wingi na kuulaki mwenge huo hakika
mwamko huu wa wananchi unaonyesha jamii ya Msalala wanajali na kuthamini mbio hizi za mwenge wa Uhuru na kuwaomba Watanzania kuiga mfano huo.Mwisho amewataka wananchi na watazania kwa
ujumla kuilinda na kuitunza miradi yote inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu kwani kwa kufanya hivyo tunakuwa tunamuunga mkono kwa vitendo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.