MSALALA YAANZA KUDHIBITI UTOROSHWAJI WA MAZAO
Halmashauri ya wilaya ya Msalala imeanza zoezi la kudhibiti njia zote zinazo tumika kutoroshea mazao ya chakula na biashara mwaka 2018 pasipo kulipiwa ushuru ambapo watoroshaji hao wamekuwa wakiikosesha Halmashauri hiyo Mapato. Katika udhibiti huo Halmashauri imeamua kujenga vizuizi mbalimbali kwenye baadhi ya maeneo yake ili kuimarisha namna bora ya ukaguzi na ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwani kwakufanya hivyo kutaongeza mapato kwa Halmashauri yetu mpaka sasa ni zaidi ya vizuizi saba tayari vimekwisha jengwa na zoezi la kujenga vizuizi vingine linaendelea..
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.