Zahanati ya ngaya iliyopo halmashauri ya Msalala ni miongoni mwa zahanati zilizopata fedha za ujenzi wa zahanati Tsh. Milioni 400 ambapo katika hatua za awali za ujenzi wa zahanati hiyo leo tarehe 07/09/2018 Halma ya Msalala imefunguwa zabuni ya kuwapata Local Fundi ambapo zoezi hilo limefanyika kwa kufuata sharia, kanuni na taratibu za manunuzi baada ya kupata kibari cha kamati ya FUM. Zoezi hilo lilifanyika katika ukumbi wa zahanati hiyo na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngaya, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala, Afisa manunuzi wa Wilaya pamoja na Local Fundi walioomba zabuni hizo. Sambamba na ujenzi wa zahanati hiyo utachangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma bora za afya pamoja na ajira za muda mfupi wakati wa zoezi la ujenzi wa kituo hicho.
Bonyeza hapa https://youtu.be/ZarFd_qduCo kutazama video
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.