MSALALA YANG’ARA MBIO ZA MWENGE 2017
Halmashauri ya wilaya ya masalala imetunukiwa kikombe pamoja na cheti cha ushindi kwa kuwa mshindi wa kwanza kanda ya pili. Kanda hii ilihusisha mikoa ya Morogoro, Tabora, Simiyu, Shinyanga, Tanga, Iringa na njombe na kuwa mshindi wa tatu kitaifa katika mbio za mwenge ambazo zilifanyika mwaka 2017. Hafla fupi ya kukabidhiwa kikombe na cheti yalifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Kahama leo tarehe 09 Juni 2018 na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwemo Naibu Waziri wa OW Sera Uratibu, Bunge , Ajira , Kazi, Vijana na wenye uremavu Mh. Anthony Peter Mavunde ,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ndg. Zainabu Teraki , Mkuu wa Wilaya Ndg Fadhir Nkurhu, Mkurugenzi wa Msalala Ndg. Simon Berege, Mkurugenzi wa Kahama Ndg Andason Msumba pamoja na watumishi mbalimbali toka halmashauri ya Msalala na Kahama katka zoezi hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala alikabidhiwa cheti pamoja na kikombe
Sambamba na hilo Mh. Anthony Mavunde alikabidhi hundi yenye thamani ya Tsh. 28720,000/= kwa SACCOS ya vijana ikiwa na lengo la kuwainuwa kiuchumi vijana ambapo fedha hizo zilitolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana inoyo ratibiwa na Wizara ya OW. Pia Mh. Mavunde aliwasisitiza vijana watumie vizuri fedha hizo ilikujiletea maendeleo
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.