Kauli hii imetolewa leo katika Risala ya mgeni rasmi MHE. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye amewakilishwa na Mkuu
wa Wilaya ya Kahama MHE.Mboni Mhita ambaye amewapongeza wawakilishi wa Viongozi wa mashirika ya UN-WOMEN, UNFPA
na KOICA kwa kuwezesha wana Msalala kuwa na vituo vya kuweza kuilinda jamii dhidi ya matukio ya unyanyasaji wa
kijinsia na kuiasa jamii kuvitumia vituo hivyo.
Kwa upande wake Daktari mfawidhi wa kituo cha Afya Bugarama DR. Kayanda amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali
ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR.Samia Suluhu za kusogeza huduma karibu
na jamii kwani Bugarama ni eneo ambalo limezungukwa na mgodi mkubwa wa dhahabu wa Bulyanhulu hivyo uwepo wa huduma
shufa ( one stop centre) kutawezesha jamii kupunguza gharama kwa kuwa huduma zote zitapatikana sehemu moja.
Nao wawakilishi wa Mashirika ya KOICA, UN-WOMEN na UNFPA katika risala zao wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania inayoongozwa na Rais DR. Samia Suluhu kwa kudumisha uhusiano mzuri na Serikali ya Japan ambao ndio wafadhili
wakuu katika majengo haya na shughuli mbalimbali zilizotekelezwa katika Mkoa wa Singida na Shinyanga. Wameongeza kusema
uwepo wa vituo hivi kutasaidia jamii kuripoti na kupatiwa utatuzi wa matatizo yanayowakabili jinsia na watoto.
Sambamba na kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa wilaya ya Kahama kwa kukubali kuunga mkono jitihada za mashirika
hayo kwani Mkurugenzi Mtendaji (W) ndg. Charles Fussi ameahidi kujenga majengo mawili ya huduma shufa (one stop center)
katika kata za Bulige na Isaka ambapo kila mwaka atakamilisha kituo kimoja kwa gharama ya Tshs. 50,000,000.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.