Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa NDG.Maganya amempongeza Mbunge wa jimbo la Msalala MHE.Alhaj Idd Kassim Idd kwa kuiwakilisha vema jimbo la Msalala na hivyo
Kuiomba Serikali kuleta fedha nyingi za kutekeleza miradi ndani ya Halmashauri ya Msalala,pia amelipongeza Baraza la Madiwani linaloongozwa na MHE.Mibako Mabubu mwenyekiti wa Halmashauri na
Timu ya Wataalamu inayoongozwa na NDG.Khamis Katimba Mkurugenzi Mtendaji (W) kwa kutekeleza miradi hiyo kwa ubora na viwango vya juu,hakika mmeitendea haki fedha iliyotolewa kwani majengo yame
pendeza.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya kwa mgeni rasmi,Injinia Magoto kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuthamini wananchi wa Halmashauri hiyo
kwa kuwa ndani ya kipindi kifupi fedha zimepokelewa za kujenga vituo vya Afya 5 katika kata za Segese,Bulige,Mwanase,Mwalugulu na Isaka.Gharama ya kujenga kituo cha Afya Bulige hadi kukamilika kwake
kitagharimu Tsh.650,000,000 na kimebakiza majengo 2 ambayo kufikia mwezi wa 5 yatakamilishwa, kwa sasa kituo hicho kinatoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na huduma ya mama na mtoto.
Nae Mbunge wa Jimbo la Msalala Alhaj Idd Kassim Idd amemshukuru Mwenyekiti huyo na viongozi aliyoambatana nao kwa kutembelea Halmashauri ya Msalala na kuona mradi wa Kituo cha Afya Bulige na kusikiliza
na kutatua kero za wananchi wa kata ya Bulige na kumwomba kufikisha shukrani za pekee za wananchi wa jimbo la Msalala kwa kuwezesha vituo vya Afya,Zahanati,Madarasa,vyoo,maji na miundombinu ya barabara
kurekebishwa kwani ukitembea ndani ya jimbo hilo kila kona miradi inaendelea kutekelezwa.
Kwa upande wao wananchi wameomba Kituo hicho cha Afya kianze kutoa huduma kwani miundombinu yote muhimu ipo,suala ambalo Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo DR. sisti Mosha ameahidi kuanza ndani ya siku 4
kwa kuwa Serikali tayari imeleta baadhi ya vifaa tiba vya kuwezesha kituo hicho kuanza kutoa huduma.Suala hili pia Mkurugenzi Mtendaji(W) amelipokea na kuagiza watumishi kuhamia tarehe 04-03-2024 na
shughuli zote zitolewe hapo.Akiahilisha Mkutano wa hadhara huo Mwenyeketi wa Jumuiya na Mjumbe wa Kamati kuu huyo ametoa rai kwa jamii kama wazazi kuitunza na kuilinda miradi yote inayotekelezwa kwa
manufaa ya vizazi vijavyo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.