Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Kahama Mh.Thomas Myonga leo katika
kikao cha Baraza la Madiwani cha kukamilisha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amesema Chama
cha Mapinduzi wilaya ya Kahama kimeridhika na namna Halmashauri hiyo inavyotekeleza ilani ya chama hicho
kwa kukamilisha miradi mbalimbali ya wananchi kwa wakati.
Mwenyekiti huyo amewapongeza wah.Madiwani,Mbunge,Mkurugenzi Mtendaji na wataalamu wote katika ngazi mbali
mbali kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mh.Rais Dr. Samia suluhu za kuiletea maendeleo jamii katika
nyanja za kilimo, elimu na afya. Mh.Thomas Myonga amesema yeye na wajumbe wake hufanya ziara ndani ya Halmashauri
pasipo kutoa taarifa lakini muda wote hukuta miradi ikitekelezwa kwa ubora na usimamizi mzuri.
Sambamba na hili Mwenyekiti huyo amewaagiza wataalamu wote ndani ya Halmashauri kwenda vijijini kutatua kero
za wananchi, suala ambalo limo katika ilani ya chama hicho. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Mh. Mibako Mabubu amemwahidi kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa na kuongeza kusema Halmashauri ya Msalala
imepokea fedha nyingi za kutekeleza miradi ya wananchi na kumwomba mwenyekiti wa CCM kumfikishia shukrani
za dhati za wanaMsalala Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.