OFISI YA MKURUGENZIMTENDAJI MADINI NA T.R.AWATOA ELIMU YA ULIPAJI WA KODI KWA WAMILIKI WA PLANTI NA WACHIMBAJI WADOGOWADOGO.
Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya msalala, ofisi ya mapato na T.R.A kwa pamoja waliitisha kikao na wamiliki wa mitamboya Uchenjuaji na wachimbaji wadogowadogo, mwezi wa sita mwanzo.
Akifungua kikao kazi hicho kaimu mkurugenzi mtendaji Ndg. Zabrone Donge aliwataka wadau hao kushirikiana na serikali kuleta maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla
Naye mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni muweka hazina wa halmashauri ya wilaya ya msalala Ndg. Masatu Mnyoro alieleza kuwa ulipaji wa ushuru kwa halmashauri ya wilaya, na ipo katika sheria ndogo anayefanya kazi za uchimbaji/uchenjuaji alipe ushuru huo ili uwezeshe kukamilisha miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya wilaya ya msalala. Mweka hazina huyo aliongeza kwa kusema Halmashauri ya wilaya ya msalala imevuka lengo katika zoezi zima la kukusanya mapato ambapo kufikia mwezi wa 4 (robo 3 ya mwaka) Halmashauri ya wilaya ya msalala ilikuwa imekusanya jumla ya Tsh 3,200,000,000 ambapo ni sawa na 102% na hivyo kuomba wote wanaodaiwa walipe madeni yao kabla ya 2016/2017 kuisha. Alihimiza ni vema kubadilika kulingana na nyakati.
Akichangia mada meneja Masoko T.R.A wilaya ya Kahama Ndg. Beatus Malo aliwashukuru wajumbe kwa mahudhulio na kuwaomba walipe kodi kwa hiari ili kuwezesha maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.