Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga bi.Zainab Telack akiongozana na Katibu Tawala (M) ndg.Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wamefanya ziara wilayani Kahama katika Halmashauri ya Wilaya ya msalala.
Katika ziara hiyo wamekagua mradi wa ujenzi wa soko na ghala la kuhifadhia mazao katika kata ya bulige.
Sambamba na hilo walikagua mradi wa maji katika kata ya Ngaya ambapo Mkuu wa Mkoa aliagiza mradi huo uanze kufanya kazi mara moja ili kuondoa tatizo la maji linalowakabiri wananchi wa eneo hilo.
Katika kata ya Segese miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya sekondari Segese pamoja na kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti vilitembelewa na kamati hiyo ilitoa ushauri wa spidi ya ujenzi huo iongezeke sambamba na kufanya ukarabati katika kiwanda cha kukamua mafuta.
Wageni hao wa Mkoa walikaribishwa na wenyeji wao Kaimu Mkuu wa Wilaya ndugu Timothy Ndanya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala ndugu Simon Berege, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya na Wakuu wa idara na Vitengo wa Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.