Serikali katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imejipanga kuondokana na utegemezi wa mapato yake
ya ndani kutegemea uzalishaji wa madini ya dhahabu unaofanywa na mgodi wa Bulyanhulu, kwani Halmashauri hiyo hupata 70% ya
mapato yake kutoka mgodi huo na 10% kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Msalala MHE. Mibako Mabubu wakati wa
ziara ya kujifunza namna ya uzalishaji wa zao la korosho katika Halmashauri ya Manyoni iliyoko mkoani Singida.
Ziara hiyo imeongozwa na Mhe. Mibako mabubu akiongozana na Baraza la waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji (W ) ndugu
Charles Fussi, na wakuu wa idara 6 wanaohusiana na shughuli za maendeleo na ustawi wa Halmashauri. Uchumi wa wananchi wa
Halmashauri ya Msalala unategemea sana uchimbaji wa madini ya dhahabu unaofanywa na mgodi mkubwa nchini wa Bulyanhulu pamoja
na wachimbaji wadodo wadogo huku makusanyo mengine kama ushuru wa mazao, leseni za biashara na magulio yanachangia 20% kwenye
pato la Halmashauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji ndg. Charles Fussi amesema ardhi ya Halmashauri ya Msalala inafanana na ardhi iliyopo manyoni
hivyo wananchi wa Msalala wachangamkie fursa hiyo pindi Halmashauri itakapoanzisha uzalishaji kwani zao la korosho lina manufaa
makubwa kwa jamii, nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni katika salamu zake kwa wanamsalala amesema zao la korosho huanza kutoa
korosho ndani ya miaka 3 na huendelea kwa muda wa miaka 30 na zaidi. Zao hili likitunza vizuri huwa na kipato cha uhakika katika
kaya.
Akitoa maelekezo kwa waheshimiwa Madiwani na wataalamu, Afisa Kilimo Halmashauri ya Manyoni bwana Kizenga Shaban amesema Halmashauri
ya Manyoni huotesha miche ya Korosho katika vitalu kwa muda wa miezi 3 na baadae huwauzia wananchi kwa Tsh. 1000 na kuwafuatilia wakulima
muda wote kwa lengo la kutoa ushauri wa kitaalamu katika uzalishaji wa zao hilo ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojito
keza. Halmashauri ya Manyoni imehusisha wadau mbalimbali waliopo ndani na nje ya nchi katika ulimaji wa zao hili hivyo ni vema pindi
uzalishaji uanzapo Halmashauri itoe matangazo kwa wadau ili kuunga mkono kilimo hicho.
Imetolewa na kitengo Cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.