Mbio za mwenge wa uhuru zimehitimishwa leo mkoani Shinyanga kwa Mkuu wa mkoa huo Bi.Christina Mndeme kuukabidhi mwenge huo,timu ya wakimbiza mwenge kitaifa na msafara wake kwa mkuu wa
mkoa wa Geita Bwana Martine Shigela katika kijiji cha Nyamholong'ho. Bi Mndeme amesema Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga ulizindua,kuona na kuweka mawe ya msingi jumla ya miradi 41 yenye
thamani ya Tshs. 14,027,687,000,000 na ulikimbizwa km.571.5 katika Halmashauri 6 na kulakiwa na maelfu ya wananchi.
Akiwaaga wananchi wa Mkoa wa Shinyanga Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg.Abdalla Shaim Kaim amesema" kwa kweli wangependa kuendelea kukaa Shinyanga lakini ratiba hairuhusu hivyo
kuahidi kurudi mara baada ya kukamilisha ratiba yao", hii imetokana na mapokezi mazuri,ukarimu na utekelezaji mzuri na wa viwango vya juu wa miradi yote ya maendeleo iliyopitiwa na mbio
hizo, hakika Mkoa wa Shinyanga mna kila sababu ya kupata hati safi umati mkubwa wa wananchi maeneo mbalimbali walikesha na Mwenge wa uhuru.Hii inaonyesha uzalendo mkubwa kwa taifa letu.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.