Shilika hili limeaanza mwaka 2016 na linatarajia kumaliza mwaka 2019, shilika linafadhiliwa na Lilian Forndation wa Uhoranzi, shirika hili linatetea haki za watu wenye Ulemavu. Mwenyekiti wa shirika hili alieleza njinsi wanavyo fanya kazi kwa ushirikiano na TAS kutetea haki za watu wenye ulemavu wa Ualbino wilayani Msalala, kwa upande wake naibu mwenyekiti muheshimiwa Benedicto mamwali wa Msalala alilishukuru shilika hilo kwa msaada wanaotoa kuwasaidia walemavu wa Ualbino wilayani msalala, kutokana na maisha waliyo kuwa wanaishi zamani na maisha wanayo ishi kwa sasa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama mheshimiwa bwana Anamringi Macha alizishukuru sana taasisi ambazo zinaendelea kujitolea kuwasaidia ili kuhakikisha maisha ya watu wenye ulemavu wa Ualbino kuwa na maisha ya kawaida na kutokujihisi kuwa wanatengwa, pia mkuu wa wilaya alisisitiza kuwa watu wenye ulemavu wa albino waache kujinyanyapaa wenyewe, wajishughulishe kulingana na hali zao.
Sekta mbalimbali nazo zilijieleza jinsi wanavyo toa misaada kwa watu hao wenye ulemavyu wa Ualbino, sekta hizo ni TASAF,CHF, sekta ya Afya Pamoja na sekta ya Elimu sekta hizi nazo zinajitahidi kuwasaidia watu wenye ulemavyu wa Ualbino kulingana na jinsi mtu mwenye ulemavu huo anatakiwa asaidiwe.
Bonyeza link hii https://youtu.be/KrrvUAcKStI kutanzama na kusikiliza
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.