Kauli hii imetolewa na Katibu wa Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji(W)
NDG. Hamis Katimba wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Msalala
ambapo amewataka Wajumbe wa Kamati hiyo, Waheshimiwa Madiwani wote na Wataalamu wa halmashauri kuwa mstari
wa mbele kuhakikisha vikundi vyote vilivyokopeshwa fedha na Halmashauri vinarejesha fedha zilizokopa ili
ziweze kutumika kwa vikundi vingine pindi Serikali itakapotoa mwongozo mpya wa ukopeshaji.
Kamati hii imetoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri unaoongozwa na MHE. Mibako Mabubu mwenyekiti wa Halmashauri
akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji (W) NDG. Hamis Katimba kwa kusimamia na kuhakikisha miradi iliyoibuliwa
inatekelezwa kwa viwango vya juu na kwa wakati. Kamati hii pia imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kutoa fedha kuwezesha ukamilishaji wa ofisi ya makao makuu ya Msalala, Hospitali ya wilaya,
ujenzi wa vituo 2 vya afya vyote vikiwa na lengo la ustawi wa afya za wananchi.
katika kikao hiki taarifa za utekelezaji wa shughuli Halmashauri za robo ya nne, wajumbe wameshauri Serikali
kuleta mbolea mapema kwani kilimo katika eneo hili huanzia mwezi wa tisa,sambamba na Halmashauri kuchagua
vituo vya uuzaji wa pembejeo vilivyo karibu na wananchi wa Msalala kwani mwaka jana wananchi walipata usumbufu
wa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma, suala hili limepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji (W) na ameahidi
kulifanyia kazi.
Kamati hii imemwomba Mkurugenzi Mtendaji (W) kushughulikia tatizo la wanufaika wa TASAF ambao wamefanya kazi
katika ajira za mda pasipo kupatiwa fedha zao licha ya tatizo hili kuwasilishwa TASAF makao makuu miezi 5 iliyopita
sambamba na orodha ya kaya maskini zilizoorodheshwa mwaka 2021 mpaka sasa hazijaingizwa kwenye mpango. Mkurugenzi
Mtendaji (W) ameahidi kumwalika Msimamizi wa TASAF(W) kwenye baraza la Madiwani ili kutoa majibu ya hoja hii.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
MSALALA
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.