Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi ya Halmashauri ya Msalala (CMAC) MHE.Frola Sagasaga ameutaadharisha umma wa wakazi wa Halmashauri ya Msalala kuchukua tahadhari
wakati wote kwani Halmashauri hiyo ina mwingiliano mkubwa wa watu ambao hufika kwa ajili ya kujitafutia ridhiki kutokana na kuwa na fursa mbalimbali.Baadhi ya fursa
hizo ni uwepo wa migodi midogo midogo ya dhahabu na kwa mwaka huu mpunga mwingi umevunwa hivyo kupelekea maeneo mengi vijijini kuwa na wageni wengi hali ambayo
inaweza kuchochea maambukuzi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.Niombe Kamati za kudhibiti Ukimwi za kata (WMAC) na Vijiji (VMAC)zifufuliwe na zisimamie suala hili katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mratibu wa Ukimwi Halmashauri ya Msalala NDG.Jackson Oswago ameunga mkono hoja hiyo kwa kutoa takwimu ambapo amesema licha ya takwimu za maambukizi kuonyesha
maambukizi ya ukimwi mkoani shinyanga yamepungua lakini ipo mikoa ambayo ilikuwa na kiwango kidogo cha maambukizi lakini kwa sasa takwimu zinaonyesha maambukizi katika mikoa hiyo
kuongezeka na maeneo yetu tunapokea watu kutoka sehemu mbalimbali hivyo ni vizuri wananchi kuchukua tahadhari katika maamuzi wanayoyafanya kwani siku hizi jamii imejisahau na
kuona ukimwi kuwa ni ugonjwa wa kawaida,tusichukulie poa ukimwi unaua na hauzoeleki chukua tahadhari Mtanzania mwenzangu kwani tu nguvu kazi ya Taifa.
Sambamba na hilo Mwenyekiti huyo wa Kamati ya kudhibiti ukimwi (CMAC) ameiagiza Halmashauri hiyo kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha vikundi vya vijana,wanawake na walemavu
vinasajiliwe ili kuweza kukidhi mahitaji ya kupewa mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri.Agizo hilo limetokana na ziara ya kamati hiyo iliyofanya tarehe 11.07.2024 ambapo
kamati ilitembelea kikundi cha vijana cha upendo wajasiriamali waliopo katika kata ya Segese na kuona shughuli wanazozifanya, moja ya shughuli hizo ni biashara ya matunda sokoni.Wanakikundi
hao wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuweka mazingira mazuri kwa mashirika mbalimbali ikiwemo SHIDEFA PLUS kwani linawawezesha kupata elimu za stadi za maisha.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.