Kauli hii imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji(W) Halmashauri ya Msalala NDG.Khamis Katimba katika kikao cha kuyajengea uwezo mabaraza ya ardhi ya Kata.Kikao hicho kimefanyika
katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mwl.Nyerere iliyopo katika kata ya Segese ambapo wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata 9 wamehudhuria na kujengewa uwezo.Mkurugenzi Mtendaji(W)
amewataka wajumbe hao kutenda haki kwa kila mwananchi kwani kazi waliyopewa ni ya kitumishi na si ya kupata faida kwani ina vishawishi lakini amewataka wasimamie haki maana malipo
yao ni makubwa mbele ya mwenyezi Mungu.
Awali Mwanasheria wa Halmashauri NDG.Leonard Mabula amesema Mabaraza ya Ardhi ya Kata yana mchango mkubwa katika kuhakikisha mashauri ya ardhi yanamalizwa katani na kuwezesha wananchi
kupata haki zao na wanaposhindwa ni sharti mashauri hayo yapelekwe mabaraza ya ardhi ya Wilaya hivyo kazi yao ni kutoa ushauri na sio hukumu kwani kazi ya kutoa hukumu ni ya mahakama
sambamba na hilo amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji(W) kwa kuona umuhimu ya mabaraza haya kujengewa uwezo kwa kukumbushwa majukumu yao ya msingi.
Kwa upande wao wajumbe wa kikao hicho wamempongeza NDG.Khamis Katimba kwa kuthamini kazi ya kila mtu ndani ya Halmashauri kwani Mkurugenzi Mtendaji huyo amekuwa akitoa elimu kwa wananchi
na wataalamu ngazi za vijiji na kata na kuwezesha wataalamu hao kuongeza hari ya utendaji kazi hasa katika sekta za kilimo,elimu,afya na uwekezaji kwani jamii sasa inawezeshwa kulima
kisasa na kupitia mafunzo haya wajumbe hao wameahidi kufanyia kazi yote waliyoelekezwa na kujiepusha na rushwa katika utoaji haki.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.