Kauli hii imetolewa na mgeni rasmi, makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Kahama mkoani Shinyanga ndugu Benedicto Manowali leo wakati wa uzinduzi wa gulio na mnada wa ng’ombe, mbuzi, kondoo na biashara ndogo ndogo katika kijiji cha bunango kata ya Bugarama. Sherehe hiyo imehudhuriwa na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala DR. Ntanwa Kilagwile, Afisa mapato ndugu Samwel Silutongwe, Kaimu mweka hazina, wataalamu mbalimbali wa kata, viongozi wa siasa na dini na umati mkubwa wa wananchi.Akiwakaribisha viongozi na wananchi katika sherehe hiyo mtendaji wa Kata ya Bugarama amesema uwepo wa gulio na mnada utasaidia kuchochea maendeleo ya wananchi na kuchangia pato la taifa kwani miundombinu ipo tayari muda mrefu ambapo eneo hili ni rahisi kufikika kwa kuwa Halmashauri wakishirikiana na mgodi wa Accacia walitengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara. Katika sherehe hii vikundi mbalimbali vya muziki wa asili vimetoa burudani na kukonga nyoyo za umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza.
Akitoa risala ya sherehe hii ya ufunguzi mgeni rasmi amesema Halmashari imeamua kuzindua gulio na mnada kwa siku ya jumapili ili kurahisisha shughuli za biashara kwa wafugaji na wakulima kwani awali mkulima alipaswa kusafiri kilomita nyingi kwenda kuuza mifugo yake, hivyo ufunguzi huu utasaidia kupunguza gharama za usafiri na kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya kata ya Bugarama na Bulyanhulu. Sambamba na hili mgeni rasmi ameongelea mapato yanayokusanywa na Halmashauri huwarudia wananchi wa Halmashauri ambapo amesema kipaumbele hutolewa kwa shughuli za kiuchumi za eneo husika hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza katika gulio na mnada huo. Ametoa mfano wa ushuru wa stendi kwa mwaka 2017/18 Halmashauri ilipanga kukusanya Tsh. Milioni 60 ambapo mpaka sasa imekusanya Tsh. Milioni 40.
Ameitaka jamii ijilinde na maambukizi mapya ya ukimwi kwani ukimwi upon a unaua, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kwenda kupima na kufahamu afya yake.
Imetolewa na Kitengo cha TEHAMA Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.