UJIO WA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI HALIMASHAURI YA KAHAMA MJI NA HALMASHAURI YA MSALALA .
Ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. Anjelina Mabula (MB) katika Halmashauri ya mji wa Kahama na Halmashauri ya Wilya ya Msalala ulikamilika baada ya kufanya mkutano na viongozi wa Halmashauri tatu ambazo ni Kahama mji, Halmashauri ya Msalala pamoja na Halmashauri ya Ushetu ambapo alipokea taarifa za halmashauri hizo kutoka idara ya ardhi pamoja na kuzungumza na Wakurugenzi pamoja na Maafisa Ardhi na kuwaeleza namna ya uboreshaji wa utendaji kazi pamoja na kuepuka usababishaji wa migogoro ya ardhi. Baada ya kumaliza mkutano wake na Wakurugenzi , Naibu Waziri huyo alikwenda kukagua eneo lenye mgogoro kati ya Wananchi na Serikali ambapo aliamua mgogoro huo na kutoa uamuzi kuwa eneo hilo litabaki kuwa ni mali ya Serikali na kuwataka wananchi kwenda mahakamani iwapo hawajalidhika na uamuzi huo . Na baada ya ukaguzi huo Naibu waziri alielekea ofisi ya masijala ya ardhi na kufanya ukaguzi ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa ardhi.
Mheshimiwa Naibu Waziri alipo maliza ukaguzi huo alimuagiza Kamishina wa ardhi Kanda magharibi kwenda kukakagua na kuzungumza na wananchi wa kata ya Isaka na kusikiliza mataizo yao na kuahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza ambapo alisema kimsingi Halmashauri ya Msalala haikuwa na mgogoro wowote wa ardhi kwa kuwa wamiliki wengi walishaenda mahakamani na hukumu kutolewa.
Naibu waziri Mh. Anjerina Mabula akizungumza na wananchi kwenye eneo lenye mgogoro katka eneo la Igomelo Kahama Mji.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.