Un women yaendelea kumwaga miradi Msalala
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala yaendelea kunufaika na miradi mbalimbali kutoka shirika la Un women ambapo leo tarehe 25 Januari 2022 imekabidhi mradi wa choo katika soko la Segese kata ya Segese na kuzinduliwa na kaimu Mkuu wa Wilaya Mh. Timoth Ndanya . Hafra hii fupi ya ufunguzi wa Mradi ilifanyika katika kata ya segese na kuhudhuriwa na Wananchi, Wataalamu toka Halmashauri ya Msalala wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Edward Charlse Fusi pamoja na wageni tok shirika la Un Women.
Akizungumza na wananchi Mkuu wa Wilayab aliwataka nanchi na wafanya Biashara wa soko hilo kushiriki kwa pamoja kulinda na kusimamia mradi huo. Pia aliwaasa wazazi kuhakikisha wanawapeleka wanafunzi wote waliofaulu shuleni ili kuendelea na masomo ya sekondari.
Sambamba na hili Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri Ndg Fusi aliwaahidi wananchi kuwa Halmashauri ya Msalala itaedelea kutoa ushirikiano na wanachi hao pamoja na kuombau kufanikisha ujenzi wa wa soko la kisasa kwani Mji wa segese unaendelea kukua kwa kasi .
Mradi huo umegharimu kiasi cha zaidi ya Tsh. Milioni 21 na hivyo utawanufaisha wakazi na wafanya biashara zaidi ya 400 ndani ya soko hilo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.