‘‘WAKANDARASI HAKIKISHENI MNATUMIA MARIGHAFI ZA NDANI KATIKA KAZI ZENU’’; PROF,MKUMBO
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Prof,Kitila Mkumbo,amewataka wakandarasi hapa nchini kutumia marighafi yanayotengenezwa na viwanda vya ndani ili kukamilisha miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali kwa wakati ulipangwa.
Alisema kuwa unapotumia marighafi kutoka nchi za nje huchelewa kufika kwa muda mwafaka na kupelekea mradi kushindwa kukamilika kwa wakati ikiwa ni pamoja na kushindwa kutoa huduma kwa wananchi ambao ndio walengwa wa miradi hiyo.
Prof.Mkumbo aliyabainisha hayo jana wakati akisaini hati ya makubaliano ya kisheria katika kutekeleza mradi wa pamoja(JOINT WATER PARTNESHIP PROJECT) unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 13.8 nautakao wahudumia zaidi ya wananchi elfu kumi kutoka mikoa ya Geita na Shinyanga.
Alisema kuwa,kila mkandarasi anatakiwa kutumia ipasanyo marighafi kutoka katika viwandani vya ndani ili iwe rahisi kukamilisha miradi kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi,huku akivitaka viwanda vya ndani kutoa marighafi zenye ubora wa hali ya juu.
“Nataka kuona kila mkandarasi anatumia marighafi kutoka katika viwanda vyetu vya ndani nasio kwenda kununua nchi za nje,tumekuwa tukipoteza muda katika kukamilisha miradi yetu tunayotekeleza kwa kusubilia marighafi kutoka nje na huku viwanda vyetu vinazalisha kila aina ya marighafi”Alisema.
Prof,Mkumbo aliongeza kuwa,”Viwanda vyetu vya ndani hakikisheni mnatengeneza bidhaa au marighafi zenye ubora wa hali ya juu,huku akiwataka mamlaka ya uthibiti ubora(TBS) kuhakikisha bidhaa hizo kama zinaubora unaotakiwa kabla ya kuingizwa sokoni.
Aidha kuhusu mradi wa pamoja prof,Mkumbo alisema,mrdi huo kwa awamu ya kwanza utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 13.8 huku Halmashauri ya Shinyanga ikitoa milioni 400,Halmashauri ya msalala Milioni 600,Halmashauri ya Nyang’hwale milioni 600, acacia Bulyanhuru ikitoa bilioni 4.5 pamoja na serikali kuu bilioni 5.2.
Nae meneja wa Migodi ya Bulyanhuru na Buzwagi Benedict Busunzu alisema kuwa,mradi huo utapita katika vijijini 14 kutoka mikoa ya geita na shinyanga na utawahudumia zaidi ya wananchi elfu kumi,nakwamba mradi huo utasaidia kumshusha mama ndoo kichwani ifikapo mwaka 2021.
Alisema, mradi huo utatoa maji kutoka ziwa Victoria kupitia mradi wa Kashwasa huku ukianzia katika kijiji cha Mhangu hadi kijiji cha ilogi na kuhudumia vijiji vyote vya njiani ambavyo ni Mwenge, Nyugwa, Mwamakiliga, Kharumwa, Izunya, kafita, lushimba, kakola, namba tisa, rwabakanga, Bushing’we na Bugarama.
Kwa upande wake meneja maradi kutoka kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) Lzangi Li alisema kuwa,asilimia kubwa ya marighafi au mabomba atatumia kutoka katika viwanda vya ndani,nakwamba zaidi ya bilioni 3.4 zimetegwa kwa ajili ya kununua vifaa hivyo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.